KATA ya Mjimwema ni miongoni mwa kata 21 zinazounda Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Kata hii inakadiriwa kuwa na jumla ya wakazi 14,951 ambapo wanaume ni 7011 na wanawake 7940. Ujenzi wa mradi wa ofisi ya kata ulianza tarehe 9/3/2012
Lengo la mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kata hiyo ni kutatua tatizo la ukosefu wa jengo la ofisi ya kata kwa sababu kata hii ni mpya iliyogawanyika kutoka kata mama ya Lizaboni.
Mradi huu hadi sasa umegharimu kiasi cha shilingi milioni 61,000,000.00,kati ya fedha hizo Halmashauri ya Manispaa imetoa zaidi ya shilingi milioni 37,,serikali kuu imetoa shilingi milioni 15 na nguvu za wananchi ni zaidi ya shilingi milioni nane.
Matarajio ya wananchi wa kata hiyo kwamba Ujenzi wa ofisi ya kata utakuwa umetatua tatizo la ukosefu wa jengo la ofisi ya kata na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi. wananchi hao wanaishukuru Halmashauri ya Manispaa ya Songea na Serikali kuu kwa kuchangia fedha za ujenzi wa ofisi hii.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Juni 13,2018.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa