Waziri wa Utamaduni, sanaa, na Michezo amewataka wananchi kutoa kero zao zinazowakabili wananchi kupitia kwenye Mitaa yao ili Serikali iweze kupokea na kutatua changamoto hizo.
Hayo yamejiri kwenye mkutano wa wananchi ambao ni mwendelezo wa ziara ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro ya kupita kata kwa kata kupokea kero za wananchi ambayo imeanza tarehe 09 Julai 2024 ambapo tayari hadi kufikia tarehe 10 Julai 2024 ametembelea kata 06 ambazo ni kata ya Mletele, Seedfarm, Bombambili, Tanga, Mshangano, na Msamala.
Miongoni mwa kero zilizotolewa na wananchi wa kata hizo ni pamoja na barabara, mifereji na madaraja, miundombinu ya shule, Maji, na malipo ya fidia ya barabara ya Mtwara Corido ambapo majibu ya mswali hayo yalitolewa na Wataalamu mbalimbali wakiwemo TARURA, TANROAD, na wakuu wa Idara mbalimbali waliohudhuria ziara hizo.
Ziara hiyo inaendelea kwa kata ya inayofuata ni Lilambo, Ruhuwiko, na Mwengemshindo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa