Manispaa ya Songea imekuwa ikiendelea na utekelezaji wa WIKI ya Maadhimisho ya sherehe za miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo na upandaji wa Miti katika maeneo ya shule, kongamano mbalimbali za vijana na wazee, kukagua miradi, Bonanza la Michezo na Usafi wa Mazingira katika maeneo ya kijamii na makazi.
Katika kutekeleza shughuli hizo Manispaa ya Songea imehitimisha Maadhimisho hayo leo tarehe 29 Aprili 2023 kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo la Soko la Bombambili kwa lengo la kuunga Mkono Maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na pamoja na kuweka mji katika mazingira ya Usafi.
Akizungumza Afisa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira Beno Philipo Mpwesa amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa, pamoja na Viongozi wa Masoko yote wahakikishe wanasimamia usafi wa Mazingira na kufanya ukaguzi wa nyumba hadi nyumba pamoja na kutumia sheria ndogo za usafi wa mazingira ambazo hutumika kwa yeyote atakaye vunja sheria ndogo hizo.
Beno aliongeza kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi hivyo ametoa rai kwa jamii kushiriki kufanya usafi hususani usafi wa mwisho wa mwezi ambao hufanyika kila ifikapo mwishoni mwa mwezi husika.
Kwa upande wao wananchi wakizungumza na chanzo hiki cha Habari wametoa maoni yao kuwa “ Muungano uendelee kudumishwa kwasababu unaleta Mshikamano, Umoja, Upendo na Amani ambao unasaidia watu kuishi kwa kusaidia na kushirikiana katika shughuli za kijamii husasani kushiriki kufanya Usafi wa Mazinngira.” Mwisho wa kunukuu.
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY,
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa