Mkuu wa wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Pololet Mgema amezindua kampeni ya jiongeze tuwavushe salama katika kata ya Ruvuma manispaa ya Songea.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mgema amesema kuwa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama ina lengo la kuongeza kasi ya uwajibikaji,kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga katika Manispaa ya Songea.
Mgema amesema takwimu ya vifo kwa mwaka 2015/2016 inaonesha kuwa viwango vitokanavyo na uzazi ni 556 kwa kila vizazi hai 100,000 ambayo ni sawa na wanawake 30 ambao hufariki kila siku nchini kutokana na matatizo ya uzazu..
Takwimu za Manispaa ya Songea kwa mwaka 2018 zinaonesha kuwa kulikuwa na vifo 22 vilivyotokea sawa na 188 kwa kila vizazi hai 100,000. Kutokana na vifo hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amewaomba wananchi kuongeza nguvu kwa kutekeleza na kusimamia ili kuokoa maisha ya wananchi.
“Maneno basi, hapa ni vitendo tu, hapa ni kazi tu, Mama akivuka salama na nchi imevuka salama.’’,alisisitiza Mgema.
Naye,Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt. Mameritha Basike ameyata malengo ya kuzindua kampeni hiyo ya jiongeze tuwavushe salama kuwa ni kutaka kupunguza vifo vya wajawazito, wazazi na watoto wachanga nchini Tanzania.
Mganga huyo amesema madhumuni ya kampeni hii ni kuhamasisha viongozi wa ngazi zote,serikali,viongozi wa Dini,Mashirika yasiyo ya kiserikali,wadau wa maendeleo,Watoa Huduma za Afya,Familia na Jamii kwa ujumla.
Kwa mujibu wa Basike, sababu zinazosababisha vifo kwa wazazi na watoto wachanga, ni kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua ambapo asilimia 18 ya vifo intokana na kifafa cha mimba na asilimia tano,kutoka damu kabla ya kujifungua na ,kushindwa kupumua ni asilimia 25.2.
Hata hivyo amezitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa uwelewa mdogo kwa jamii kuhusu masuala ya Afya ya Uzazi kwa Mtoto,akina mama wanachelewa kuanza kliniki mapema na uhaba wa magari ya kubebea wagonjwa.
Dkt.Basike ameitaja mikakati madhubuti ambayo wameweka kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na mtoto, kuwa ni kuimarisha huduma za uzazi wa mpango zikiwemo huduma za ushauri kwa wanawake mara baada ya kujifungua,utoaji wa Elimu ya Afya ya uzazi kwa jamii na ushirikishwaji wa wanaume katika huduma za uzazi.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea ina jumla ya vituo 40 vinavyotoa huduma za Afya,kati ya vituo hivyo Hospitali moja,vituo vya Afya vinne na Zahanati 35
Imeandaliwa na
Farida mussa
Kitengo cha TEHAMA Manispaa
Agosti 16,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa