JUMLA ya wanawake 40 kati ya 1849 waliopimwa saratani ya shingo ya kizazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamegundulika kuugua saratani hiyo.
Kulingana na uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi ambao umefanyika katika kipindi cha kuanzia Julai 2017 hadi Juni 2018 katika Manispaa ya Songea,wanawake hao waliogundulika ni sawa na asilimia 2.2 ambapo jumla ya wanawake walipimwa matiti walikuwa ni 5319.
Hata hivyo kwa mujibu wa uchunguzi huo,wanawake 105 walidhaniwa kuwa na saratani ya shingo ya kizazi wamefanyiwa tiba mgando Na wanawake 1,819 waligundulika kuwa hawana shida yoyote.
Katika utekelezaji wa shughuli za kudhibiti UKIMWI katika kipindi cha kuanzia Julai 2017 hadi Juni 2018 ,takwimu zinaonesha kuwa watu 85,644 walijitokeza kupima virusi vya UKIMWI kati yao wateja wapya 3,873 waligundulika kuathirika na kuanzishiwa dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI ARV.
Katika kipindi hicho jumla ya akinamama wajawazito na wanaonyonyesha 495 waligundulika kuwa na virusi vya UKIMWI ambapo katika kipindi hicho jumla ya wanaume 11,494 walifanyiwa tohara ili kupunguza hatari ya kupata maambukizo ya VVU.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 4,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa