AWAMU ya pili ya mgawo wa pikipiki 10 kati ya 21 zilizotolewa kwa Waratibu Elimu 21 wa kata 21 zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma zimekabidhiwa leo katika viwanja vya ofisi ya Manispaa ya Songea.
Waratibu Elimu Kata 11 tayari walikabidhiwa pikipiki 11 katika awamu ya kwanza.Pikipiki hizo zimetolewa kwa waratibu elimu kata 2894 katika nchi nzima lengo likiwa ni kuzitumia kusimamia maendeleo ya elimu katika shule zilizopo katika kata zao.
Serikali imetoa pikipiki hizo pia kuhakikisha kuwa waratibu elimu kata wanasimamia mahudhurio ya wanafunzi katika shule ili kupunguza utoro wa wanafunzi hali ambayo itachangia kuboresha elimu kwa kuinua kiwango cha ufaulu.
Pikipiki zote katika nchi nzima zimegharimu zaidi ya shilingi bilioni 8 na milioni 576 ambazo zimetolewa kwa msaada wa wadau wa maendeleo ambao Shirika la Global Partnaship in Education kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Septemba 12,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa