MKUU wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema operesheni ya kuwasaka wanafunzi wa madarasa ya awali,msingi na sekondari ambao hawajaripoti shule itafanyika nyumba hadi nyumba ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaripoti shuleni.
Amesema uchunguzi umebaini kuwa bado kuna idadi kubwa ya wanafunzi waliotakiwa shuleni lakini bado wapo mitaani wakati serikali inatoa elimu bure kuanzia msingi na sekondari kuhakikisha watoto wote wanapata elimu.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Wilaya takwimu zinaonesha kuwa wanafunzi wa madarasa ya awali walipo shuleni hivi sasa ni asilimia 68 ya walioandikishwa ambao ni 4395 kati ya wanafunzi 9485 waliotarajiwa kuanza elimu ya Awali mwaka huu.
Amesema katika elimu ya msingi wanafunzi walioripoti darasa la kwanza ni asilimia 81 ambayo ni jumla ya wanafunzi 5425 ambapo wanafunzi waliotarajiwa kuanza shule ya msingi ni 6313.
“Hali bado ni mbaya pia hata katika elimu ya sekondari,kwa sababu wanafunzi waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu ni 3923,hata hivyo walioripoti ni wanafunzi 2726 hadi sasa sawa na asilimia 69,ni lazima tufanya msako kuwatafuta ili kujua hawa wanafunzi wako wapi ili waende shuleni’’,anasisitiza Mkuu wa wilaya.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa