JUMLA ya watalii 22 kutoka barani Ulaya kwa mara ya kwanza wamefanikiwa kufanya aina mpya ya utalii nchini Tanzania,baada ya kutumia mitumbwi kusafiri katika mto Ruvuma kupitia Hifadhi ya Taifa ya asili ya Mwambesi iliyopo kando kando mwa mto Ruvuma wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Watalii hao wametumia siku kumi kusafiri zaidi ya kilometa 160 ndani ya mto Ruvuma.Aina hii ya utalii wa kuteleza kwa mitumbwi katika mto ni ya kwanza kufanyika nchini Tanzania.Hata hivyo utalii wa kuteleza kwenye mito umekuwa unafanyika katika nchi za bara la Ulaya,Marekani na nchi ya Afrika ya kusini.
Akizungumza katika hafla ya kuwaaga watalii hao baada ya kumaliza safari yao,Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Julius Mtatiro amesema utalii katika wilaya ya Tunduru na Mkoa wa Ruvuma umefunguka rasmi na kwamba wilaya ya Tunduru ina vivutio vingi vya utalii ambavyo vinatakiwa kuibuliwa na kutangazwa katika vyombo vya habari na mitandao ili kuhakikisha kuwa wageni wa ndani na nje ya nchi wanapata taarifa sahihi ili waweze kufika na kuongeza pato la Taifa kupitia sekta ya utalii.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa