WATALII 50 kutoka nje ya nchi wanatarajia kufanya utalii katika chanzo cha Mto Ruvuma ambacho kinaanzia katika milima ya Matogoro iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Afisa Maliasili na Utalii mkoani Ruvuma,Afrikanus Challe amesema watalii hao wanatarajia kuanza utalii kuanzia Agisti 12 hadi 22 mwaka huu na kwamba watafanya utafiti kwa kufuatkia mto huo maarufu duniani kluanzia kwenye chanzo hadi unapomwaga maji yake katika Bahari ya Hindi.\
Milima ya Matogoro ndiyo chanzo cha mito mitatu maarufu hapa nchini ukiwemo Mto Ruvuma ambao unamwaga maji yake Bahari ya Hindi,Mto Ruhuhu ambao unamwaga maji yake katika ziwa Nyasa na Mto Ruegu ambao unapeleka maji yake katika mto Rufiji ambao pia unamwaga maji yake Bahari ya Hindi.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa