WATALII 50 toka nchi 16 duniani wameamua kufanya mkutano wao mwaka wa kimataifa katika Hifadhi ya Taifa ya mazingira asilia ya Mwambesi iliyopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha miezi miwili mkoa wa Ruvuma kupata makundi makubwa ya watalii kutoka nchi za Ulaya,Asia,Amerika na barani Afrika hivyo kufanya jumla ya watalii 77 kutembelea Hifadhi hiyo ambayo imepandishwa hadhi kuwa ya kitaifa.
MSITU wa Hifadhi wa Taifa wa mazingira asilia Mwambesi ulianzishwa mwaka 1956 na ulipandishwa hadhi kuwa msitu wa Taifa katika kipindi cha mwaka 2017/2018. hadhi ili kuongeza uhifadhi zaidi kutokana na kuwa na utajiri wa viumbe vya kipekee duniani wakiwemo wanyama,ndege na mimea.
Maximilian Jenes Meneja Miradi ya Palms Foundation anasema Mkoa wa Ruvuma umepokea watalii 50 toka nchi 16 duniani ambao wamefika kama watalii na pia kuendesha mkutano wa kimataifa ndani ya hifadhi ya Taifa ya Mwambesi.
“Mkutano huu wa kimataifa unahusiana na wadau viongozi wanaoongoza masuala ya uhifadhi duniani kutoka mataifa mbalimbali ,pia watajadili na kuonesha fursa mbalimbali zinazotokana na uhifadhi’’,anasisitiza Jenes.
Anasema mkutano huo unalenga kuonesha Dunia fursa mbalimbali zinazotokana na uhifadhi na kwamba wananchi,wanajamii wanaozunguka hifadhi ya Mwambesi na Taifa kwa ujumla wataweza kunufaika kupitia ziara ya watalii hawa wa kimataifa.
Hata hivyo Jenes anasema mikutano ya namna hii imefanyika katika nchi mbalimbali za Afrika na kwamba kwa Tanzania hii ni mara ya pili kufanyika mkutano wa kimataifa kama huu,ambapo kwa mara ya kwanza ulifanyika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa