MKURUGENZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Tina Sekambo amewasainisha mikataba ya lishe watendaji wa wata 21 zilizopo katika Manispaa hiyo ili kupunguza tatizo la utapiamlo na udumavu katika Halmashauri hiyo.
Mikataba hiyo imesainiwa kwenye ukumbi wa ofsi ya Mkuu wa wilaya ya Songea na kushuhudiwa na Mkuu wa wilaya hiyo Pololet Mgema.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Tina Sekambo amesema suala la lishe ni la Kitaifa hivyo amewaagiza watendaji hao waende kutekeleza kwa vitendo ili kupunguza upiamlo na udumavu ambao unachangia umaskini na kuathiri makuzi ya watoto ambao ni Taifa la kesho..
Akizungumza baada ya watendaji hao kusaini mikataba, Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema katika wilaya ya Songea hakuna sababu ya kuwa na utapiamlo na udumavu kwa kuwa wilaya hiyo imezalishsa aina mbalimbali za vyakula yakiwemo matunda ya aina mbalimbali.
“Tunataka kuondoa udumavu, mtendaji yeyote ambaye hatatimiza wajibu wake, katika kusimamia mikataba ya lishe tutamchukulia hatua”. Amesema Mgema.
Amesema ili suala la lishe liweze kufanyika vizuri imewekwa mikataba ya usimamizi wa kazi ambayo imesainiwa katika ngazi ya kitaifa, mkoa, wilaya, na sasa katika halmashauri ambapo watendaji wa kata wamesaini na itasainiwa pia na watendaji wa mitaa yote 95 ya Manispaa ya Songea.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya songea Dkt Mameritha Basike ameyataja malengo yanayotekelezwa katika mkataba huo kuwa ni kufanikisha suala la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika jamii na kuhakikisha kuwa jamii kupitia uongozi wa mtaa inashiriki ipasavyo katika kupanga,kutekeleza na kufutilia maendeleo ya utekelezaji wa mpango na afua za lishe.
Basike ameyataja majukumu sita katika upimaji wa utendaji kazi katika kukabiliana na utapiamlo,Kuhakikisha lishe ni ajenda ya kudumu katika vikao vva kisheria vya kamati ya maendeleo ya kata, Kuchochea na kuibua fursa za lishe, matatizo na suluhu za kutatua matatizo ya lishe na kuhakikisha vipaumbele vinajumuisha afua za chakula na lishe, afya, maji safi, usafi wa mazingira na uchangamshi kwa watoto wadogo.
Ameyataja majukumu mengine kuwa ni Kukusanya, kuthamini na kujadili taarifa za lishe kutoka kwenye kaya, Kuhakikisha wadau wa lishe wote waliopo kwenye mtaa wanatambulika na wanawasilisha taarifa zao kwenye kamati ya maendeleo ya mtaa na Kufanya ufuatiliaji wa shughuli za lishe na kutolea taharifa.
Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa mikoa mitano inyoongoza kwa udumavu na utapiamlo Tanzania.
Imeandikwa na Farida Mussa
Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Julai 31,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa