Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile ametoa siku 14 kwa Maafisa Watendaji Kata, Mitaa na Maafisa Elimu Kata kuhakikisha wanakamilisha zoezi la kuwapata wanafunzi 469 wasioripoti shule ikiwa wanafunzi 6343 waliochaguliwa kujiunga kidato kwanza 2023 kati ya hao ni Wanafunzi 5874 wameripoti shule.
Amewataka kutumia mbinu shirikishi jamii ili kufanikisha kuwapata wananfunzi wote ambao bado hawajaripoti pamoja na kubaini changamoto ambazo zinapelekea Mwanafunzi kutoripoti shule kwa wakati husika.
Aidha, ametoa Rai kwa Wataalamu hao kuwajibika kila mtu katika eneo lake na ameahidi kutoa Zawadi kwa Mtendaji yeyote atakaye fanikisha kwa asilimia 100% kusimamia zoezi la wananfunzi wasioripoti shuleni.
Kauli hiyo imetamkwa leo katika kikao kazi cha Maafisa Watendaji Kata 21, Maafisa Watendaji wa Mitaa 95, Maafisa Elimu Kata 21, Wakuu wa Idara kilichofanyika katika ukumbi wa Shule ya Wasichana Songea kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa wanafunzi wa kidato cha kwanza ambao wameripoti na wasioripoti Manispaa ya Songea.
Mhe. Ndile amewataka Watendaji wa Serikali za Mitaa kuandaa Mpango shirikishi ambao utatekelezeka katika kufanikisha utoaji wa chakula shuleni ambapo amesema ni asilimia 63% za shule ambazo zinatoa chakula kwa wananfunzi wakati wa masomo.
Kwa upande wa Afisa Elimu Sekondari Janeth Moyo amesema Mansipaa ya Songea imeweka Mkakati wa kuhakikisha wanatumia mbinu mbalimbali ikiwemo na sheria ndogo ili kufanikisha kuwapata wanafuzi wasioripoti.
IMEANDALIWA NA,
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa