Halmashauri ya manispaa ya Songea imeanza kampeni ya utoaji wa chanjo ya kuzuia Saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wenye umri wa miaka 9 hadi 14 ambayo imeanza kufanyika kuanzia tarehe 22 hadi 28 Aprili 2024 kwa walengwa 22,550 wanaotakiwa kuchanjwa.
Akizungumza Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Chanjo hiyo alisema “ Lengo la chanjo ni kuzuia kabla ya kupata ugonjwa wa Saratani ya shingo ya kizazi huku akiwataka mabinti kuchoma chanjo hiyo ambayo haina madhara yoyote mwilini.” ‘Alisisitiza.’
Kauli hiyo imetolewa wakati wa ufunguzi uliofanyika shule ya Msingi Chief Mbano iliyopo kata ya Ruvuma ambapo watoto 204 walichanjwa katika uzinduzi huo.
Mganga Mkuu Manispaa ya Songea Amos Mwenda alisema “kampeni hii imelenga kutoa huduma ya chanjo ya kuzuia Saratani ya Shingo ya kizazi kwa watoto wenye umri wa miaka 9 hadi 14 hususani wanafunzi walioko shuleni Sekondari na Msingi na walioko kwenye jamii.”
Zoezi hilo linaendeshwa na watoa huduma wa afya ya Msingi pamoja na Walimu wa afya wa kila shule husika.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa