WATUMISHI 49 wa Manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma, wamenufaika na mafunzo ya yanayohusu uandaaji wa mipango na bajeti kwa njia ya mfumo wa mtandao wa kieletroniki .
Watumishi hao walipata mafunzo hayo kwa njia ya nadharia na vitendo kuendelea katika Chuo cha Ualimu cha Songea kilichopo Matogoro mjini Songea.
Mafunzo hayo yamefanyika katika nchi nzima yakiziuhusisha Halmashauri zote nchini.Mafunzo hayo ni lazima katika Halmashauri zote kwa sababu bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019 imefanyika kwa njia ya mfumo wa mtandao kuanzia Idara,Halmashauri, mkoa na hatimaye kuunganishwa TAMISEMI na kupata bajeti ya kitaifa.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa alizindua mfumo huo mpya Septemba 5 mwaka 2017 mkoani Dodoma ambapo aliagiza mfumo huo ambao umebainika utapunguza gharama za mbalimbali za uendeshaji, zikiwemo malipo ya kusafirisha wakuu wa Idara ,Vitengo na wahasibu s zitaondolewa.
Waziri Mkuu , aliagiza mfumo huo kufundishwa katika nchi nzima na umeanza rasmi kutumika katika kuandaa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2018/2019.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa Songea
Septemba 24,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa