AFISA Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Songea mkoani RUVUMA Lewis Mnyambwa amewatahadharisha watumishi wapya kuwa makini na mikopo inayotolewa na baadhi ya Taasisi za fedha badala yake amewashauri kukopa katika Taasisi za serikali kama Benki ya NMB ambayo mishahara ya watumishi wengi inapitia huko.
Mnyambwa alikuwa anazungumza katika Kikao kazi cha watumishi wapya zaidi ya 100 ambao wameajiriwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017.Katika kikao hicho mada mbalimbali zimefundishwa zikiwemo kanuni za maadili ya utendaji katika Utumishi wa umma,HAKI,wajibu na stahili za watumishi wa umma,mfumo wa upimaji wa utendaji kazi katika Utumishi wa umma na mwongozo wa mavazi katika Utumishi wa umma.
Watumishi hao pia wamepewa elimu kuhusu mikopo mbalimbali ambayo inatolewa na Benki ya serikali ya NMB ambayo inatumika na wafanyakazi wengi wa serikali.
Imeandikwa na Albano Midelo
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa