WAWAKILISHI wa Benki ya Dunia wamefanya ziara katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea na kukagua miradi mitano ambayo inatekelezwa katika Manispaa hiyo.
Wawakilishi hao wameongozana na wawakilishi wa Wizara ya TAMISEMI na wataalam kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kutembelea miradi ambayo inafadhiliwa na Benki ya Dunia.
Miradi ambayo imetembelewa ni mradi wa bustani ya Manispaa ambao umegharimu shilingi milioni 399 ambao umekamilika kwa asilimia 100 na mradi wa kituo cha mabasi cha Mfaranyaki ambao umegharimu zaidi ya shilingi milioni 576 ambao umekamilika kwa asilimia 100 na unafanyakazi.
Miradi mingine ambayo imetembelewa ni mradi wa ujenzi wa stendi mpya ya Shule ya Tanga ambao umegharimu zaidi ya shilingi bilioni sita ambao ujenzi wake umefikia asilimia 35 na kwamba mradi huo unatarajia kukamilika Septemba 2019 na wa ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilometa 10.3 ambao unagharimu zaidi ya shilingi bilioni 10 ambao ujenzi wake umefikia asilimia 40 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2019.
Miradi mingine ambayo imetembelea na Benki ya Dunia ni mradi wa machinjio ya kisasa katika eneo la Shule ya Tanga ambao umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 3.2 ambao unatarajia kukamilika Desemba mwaka huu ambapo hadi sasa mradi umefikia zaidi ya asilimia 65.
Wakizungumza mara baada ya kukagua miradi hiyo,wawakilishi hao wameipongeza manispaa kwa utekelezaji wa miradi hiyo ambayo baadhi imekamilika kwa asilimia 100 na kuagiza miradi ambayo haijamilika na kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi ili kukamilisha kwa wakati.
Pia wameagiza miradi ambayo imekamilika lakini inakabiliwa na changamoto ukiwemo mradi wa bustani ya Manispaa ya Songea,kuhakikisha wanatatua changamoto ya maji kwa kuchimba kisima ili bustani iwe ya kijani wakati wote na kuvutio wageni wanaotembelea hapo.
Katika kipindi cha mwaka 2013/2014 na 2017/2018 Manispaa ya Songea kupitia ULGSP imepewa fedha zaidi ya bilioni 27 na kwamba hadi kufikia Septemba 2018 manispaa hiyo imetumia zaidi ya bilioni 15 sawa na asilimia 56 ya fedha ilizopokea.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Oktoba 23,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa