Mwenyekiti wa Wazee Mkoa wa Ruvuma katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Alezian Nyoni amefurahishwa na kitendo cha wazee kujikita kwenye ujariamali baada ya kustaafu.
Akizungumza na wazee katika uwanja wa Zima moto mjini Songea, Nyoni amesema wazee kujishughulisha na biashara mbali mbali kunawasaidia kuimalisha afya zao na kuwasihi wazee kwenda kupima afya zao mara kwa mara ili kutambua magonjwa ambayo yanawasumbua.
“Safari ya kuelekea uzeeni haina budi kuwa na usawa na haki kwa sababu uzee haukwepeki kwa mtu yeyote leo utakuwa kijana ila kesho utakuwa mzee kwa hiyo tuwaheshimu wazee kwa maana wamefanya mengi katika kuchangia Taifa letu’’,alisisitiza.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Sophia Mfaume Kizigo amesema wazee wanaishi muda mrefu kutokana huduma za afya kuboreshwa katika uongozi wa awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli.
Kizigo amesema amesema ni vizuri wazee kwenda kuchukua vitambulisho vya ujasiriamali ili kuepuka usumbufu na kwamba Rais ameona ni vyema kuwasaidia wajasiriamali waweze kuepukana na kero ya kulipa mapato makubwa kwenye Halmashauri.
Kwa upande wake Afisa Ufuatiliaji na Tathimini wa PADI Simon Komba amesema Taasisi yao ni kusaidia masikini na wasiojiweza kama kutoa mikopo ya fedha mifugo pia kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wazee na kuwajengea uwezo wa kufuatilia haki zao katika sekta mbali mbali.
Komba amesema PADI wanawaunganisha wazee kwenye taasisi mbali mbali za kifedha kama bajeti ya kuwawezesha wazee wanawake kiuchumi kwa kuwapa mikopo kwa ujumla wa wazee wote.
Mzee Boniventula Ngonyani miaka 75 amesema mkazi wa mjimwema amefurahishwa na Serikali kuweka siku ya wazee duniani ingawa amesema kuna changamoto zinazowakabili wazee ikiwemo upatikanaji wa mbolea na matibabu kwa wazee.
“Naiomba Serikali ya awamu ya Tano iendelee kutafutia changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee wa Tanzania’’,alisema Ngonyani.
Mzee Bernadetar Hyera miaka 61 mkazi ameiomba serikali kuwakumbuka wazee ambao wamesahaulika katika huduma za afya.
Imeandikwa na Farida Mussa
Kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Oktoba 2,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa