• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Songea Municipal Council
Songea Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Songea

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto
      • Planning,Statistics and Monitoring
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafi
      • Maji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Arthi na Mipangomiji
    • Vitengo
      • Uchaguzi
      • Legal Services
      • Mawasiliano, Habari na Teknolojia
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma zetu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi isiyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZIRI aagiza kutumia Force Account kutekeleza miradi ya Wizara ya Afya

Tarehe ya kuwekwa: January 9th, 2019

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amewaagiza watendaji wa Halmshauri zote nchini kutotumia wakandarasi katika kutekeleza  miradi inayohusu Wizara  bali kutumia mtindo wa 'Force Account' yani mafundi wa kawaida katika kutekeleza miradi hiyo.

Ametoa agizo hilo mkoani Ruvuma wakati alipotembelea na  kujionea ukarabati na ujenzi katika Chuo cha Wauguzi Songea na Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Naibu Waziri huyo amefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa ya kuanza kwa mchakato wa ujenzi wa baadhi ya madarasa na ukuta wa Chuo cha Waganga mkoani humo ambao ungegharimu zaidi ya Shillingi 900 ambazo fedha hizo zingetumia mtindo wa 'Force Account' zingejenga zaidi madarasa hayo na ukuta.


Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa katika zama hizi za Serikali ya Awamu ya Tano itazingatia na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha za miradi ya Maendeleo na yeye kama Naibu Waziri ataisimamia kwa karibu Miradi hiyo.Amesisitiza kuwa ujenzi wote wa miradi utakaohusu Idara Kuu Maendeleo ya Jamii utazingatia utaratibu wa 'Force Account' na kibali cha wakandarasi kitatolewa na Mawaziri pekee na sio vinginevyo.

"Niseme tu ni marufuku kutumia wakandarasi katika kutekeleza miradi inayohusu Wizara hii niliyopo labda muyafanye haya wakati mimi sipo" alisisitiza Dkt. Ndugulile.Akitoa taarifa ya ujenzi na ukarabati wa Chuo cha Wauguzi Songea Kaimu Mkuu wa Chuo hicho Dkt Geofrey Mdodo amesema Chuo kinakabiliwa na changamoto za miundombinu na upungufu wa wakufunzi ambapo mpaka sasa kuna wakufunzi saba wanaofundisha jumla ya wanafunzi 105.

Wakati huo huo Naibu Waziri Ndugulile ametembelea na kukagua ujenzi na ukarabati wa madarasa na mabweni na mradi wa maji katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Songea.Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali imedhamiria kuzalisha wataalam katika kuwaletea Maendeleo hasa wataalam wa Maendeleo ya Jamii ikiwa ni kada muhimu katika mstakabali wa Maendeleo ya taifa letu.

Dkt. Ndugulile amewasihi wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuamsha ari ya wananchi katika shughuli za Maendeleo kushirikiana  na Serikali katika kutekeleza miradi ya Maendeleo."Niseme Kada hii ya Maendeleo ya Jamii ni muhimu Maafisa Maendeleo ya Jamii tuamshe ari na Jamii wajue jukumu la kujiletea Maendeleo ni la wananchi na Serikali na sio Serikali pekee" alisisitiza Dkt. Ndugulile.


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea  Mhe.Pololeti Mgema amemuahidi Naibu Waziri kusimamia uendeshaji wa Chuo hivyo vilivyopo katika Wilaya yake kwa ukaribu.Akitoa taarifa miradi ya ukarabati wa madarasa, mabweni na ujenzi wa miradi wa maji katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Mlale Mkuu wa Chuo hicho Bi. Luciana Mvula amesema kuwa ukarabati wa Ofisi kwa mwaka 2016/2017 uligharimu shillingi millioni 91, ukarabati wa mabweni na vyoo umegharimu shillingi Millioni 152 na ujenzi wa mradi wa kusukuma maji uliogharimu shillingi millioni 3.

Wakizungumza baadhi ya wananchuo na Watumishi wameiomba Serikali kuongeza wakufunzi na wafanyakazi katika Chuo hicho ili kuendana na mabadiliko ya mtaala uliopo.

Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile yupo mkoani Ruvuma kwa ziara ya Siku mbili kufuatilia utekelezaji katika Sekta ya Afya na Maendeleo ya Jamii nchinI.

Imetolewa na Afisa Habari Wizara ya Afya


Matangazo

  • TANGAZO LA LESENI ZA BIASHARA January 22, 2025
  • TANGAZO la usafi wa mazingira Jumamosi ya mwisho wa mwezi Septemba 2024 February 27, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Yafanikiwa Kurejesha Mil. 9.2, na Kudhibiti Mianya ya Rushwa.

    May 30, 2025
  • TAKUKURU Ruvuma Yawezesha kupatikana fedha za makusanyo Songea Dc

    May 30, 2025
  • ALAT Ruvuma na Baraza la Madiwani la Chalinze Watembelea Manispaa ya Iringa Kujifunza Ukusanyaji wa Mapato.

    May 29, 2025
  • ISMAIL ALI MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI

    May 15, 2025
  • Tazama zote

Video

ALAT RUVUMA ZIARANI IRINGA TC
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Ruvuma Region Website
  • Songea diistrict websites
  • Madaba District Council Website
  • Tunduru District Website
  • Namtumbo District Website
  • Nyasa District Website
  • Mbinga Town Council Website
  • Mbinga District Council Website
  • Songea Municipal face book

Tovuti Mashuhuri

  • Wizara ya Fedha
  • TAMISEMI
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • National Bureau of Statistics
  • Baraza la Mitihani Tanzania

Idadi ya Wasomaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    SONGEA MUNICIPAL COUNCIL

    Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA

    Simu ya Mezani: 025 2602970

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: info@songeamc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa