WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Said Jafo ametoa rai kwa wanahabari kuviibua na kuvitangaza vivutio vya utalii ili kukuza Utalii wa ndani ambao unachangia kukuza pato la Taifa.Waziri Jafo alikuwa anazungumza na maafisa habari na Mawasiliano serikalini karibu 300 kutoka nchi nzima wakati anafunga kikao kazi Ijumaa iliyopita kwenye ukumbi wa AICC Jijini Arusha .Serikali kupitia sekta ya Utalii imejipanga kuhakikisha inakusanya mapato ya kiasi cha Dola za Marekani bilioni 2.1 ifikapo mwaka 2025.Takwimu zinaonesha kuwa sekta ya utalii inaongoza kwa kuingizia nchi fedha za kigeni kiasi cha Dola bilioni mbili za Marekani kwa mwaka ambapo mwaka 2015 Takwimu zinaonesha kuwa Tanzania ilipokea watalii wa kimataifa zaidi ya milioni 1.137,mwaka 2016 watalii waliongezeka na kufikia milioni 1.284.Sekta ya Utalii inakadiriwa kuajiri watu wasiopungua 500,000 nchini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa