Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya siku nne katika mkoa wa Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme akizungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea,amesema Waziri Mkuu anatarajia kuwasili katika uwanja wa ndege wa Songea Januari pili,2019,majira ya saa kumi jioni.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,mara baada ya Waziri Mkuu kuwasili mjini Songea atasomewa taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma na Januari tatu ataanza ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Akiwa katika Halmashauri hiyo,atakagua miradi ya soko la mazao OTC Lilambo,miradi ya maji na zanahati katika kijiji cha Lugagara na mradi wa maji katika kijiji cha Muungano Zomba na hatimaye atafanya mkutano wa hadhara na wananchi katika kijiji cha Lugagara.
Kulingana na ratiba hiyo,Waziri anatarajia kuanza ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Januari 4,2019 ambako atakagua miradi na kufanya mkutano na wadau wa zao la kahawa na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Nyoni.
Waziri Mkuu anatarajia kuzindua mashine ya kisasa ya X-Ray katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea siku ya Januari 5,2019.
Mndeme ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo msafara wa Waziri Mkuu utapita kuanzia uwanja wa ndege na maeneo mengine katika wilaya ya Songea na Mbinga.
Imeandaliwa na Albano Midelo
Afisa Habari Songea Songea
Desemba 31,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa