Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe anatarajia kuwasili leo 12/08/2020 ndani ya manispaa ya Songea akitokea Wilaya ya Tunduru.
Mwakyembe atakuwa na ziara ya siku mbili kuanzia 12-13/08/2020 ambapo katika ziara hiyo atatembelea maeneo ya urithi wa ukombozi leo saa nane mchana.
13.08.2020 atatembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, pia atatembelea Mitambo ya utangazaji ya TBC na baadhi ya vituo vya binafsi vya Redio. Kisha atakuwa na mkutano wa wadau wa Habari wa Mkoa wa Ruvuma.
Mkurugenzi wa manispaa ya Songea Tina Sekambo kwa niaba ya wananchi wa Manispaa ya Songea anamkaribisha Mh. Waziri wa Habari, Sanaa, na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe katika Mji wa Songea.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY,
KAIMU AFISA HABARI – MANISPAA YA SONGEA.
12.08.2020
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa