“Utoaji wa taarifa kwa umma ni Takwa la Kisheria, Viongozi wa Umma na Maafisa Habari Tuwajibike”
Ni kauli mbiu iliyotolewa katika mkutano wa 15 wa kikao kazi cha maafisa habari, Mawasiliano na uhusiano wa Serikali kinachofanyika Jijini Mbeya kuanzia leo tarehe 24 hadi 28 Mei 2021 katika ukumbi wa chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya “MUST” na kuhudhuriwa na Maafisa Habari 370 ikiwa kati ya hao Maafisa Habari 20 kutoka Zanzibar.
Mgeni rasmi katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, na michezo, na kupokelewa na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Dkt. Hassani Abbas pamoja na Sektariet ya TAGCO na kisha kukagua vibanda vya maonesho mbalimbali chuoni hapo na kupata maelekezo ya huduma zitolewazo katika eneo hilo.
Bashungwa alisema lengo kuu la kikao kazi cha maafisa Habari, Mawasiliano na uhusiano wa Serikali limejikita katika kutekeleza kauli mbiu ambayo ni utoaji wa taarifa kwa umma ni takwa la kisheria, Viongozi wa umma na Maafisa Habari tuwajibike,” ambapo miongoni mwa mambo ambayo Serikali inasimamia ni pamoja na namna ya utaoaji habari kwa jamii.
Alisema moja ya kazi ya Afisa habari wa Serikali ni pamoja na kutangaza Miradi ya Serikali, kazi zote zilizotekelezwa na Serikali ili kuihabarisha umma iweze kufahamu jitihada zilizofanywa na Serikali yao.
Amezitaja baadhi ya changamoto zinazokwamisha utendaji kazi wa Maafisa Habari ni kutoshirikishwa kwenye vikao mbalimbali vya Taasisi, kutotengewa bajeti ya Habari na Mawasiliano, kukosa bando la internet, kutokuwa na vifaa au vitendea kazi vyenye ubora.
Amewataka Waajiri wote nchini kutenga bajeti ya ununuzi wa vifaa bora vya Afisa habari kama Kompyuta, Kamera, vinasa sauti, ili aweze kufanya kazi kwa kiwango kinachostahili ikiwemo na upatikanaji wa picha nzuri za miradi ya Serikali zenye kiwango pamoja na kutengewa bando la internet kwani Afisa Habari mara nyingi huendelea kufanya kazi wakati wowote hata nje ya ofisi na baada ya masaa ya kazi. Mhe. Bashungwa alisisitiza.
Ametoa wito kwa Viongozi wote kuhakikisha wanatatua changamoto zote zinazokikabili kitengo cha Habari na Mawasiliano ili kuwezesha jamii kupata habari sahihi, na kwa wakati sahihi na zenye tija kwa jamii na Serikali.
Amesema pamoja na uwepo wa changamoto za ukosefu wa vitendea kazi amewataka Maafisa Habari hao kuendelea kufanya kazi kwa kujituma kwani anatambua uwepo wa baadhi ya maafisa habari ambao hawajitumi kufanya kazi kwenye maeneo yao kwa kigezo hawana vitendea kazi.
Ameshauri wasimamizi wa mfumo wa EGA kwa kipindi kijacho kufuatilia Maafisa Habari ambao wanafanya kazi vizuri kwenye Website zao wachukuliwe majina yao ili waweze kupata zawadi ya kufanya kazi vizuri na zenye tija kwa jamii na serikali.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewataka maafisa habari wote kuwa makini katika kusikiliza maelekezo yanayotolewa na wawezeshaji hao ili yaweze kuwasaidia katika kuboresha utendaji wa kazi na kutangaza miradi yote ya Serikali.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
24.05.2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa