Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji Mhe. Hussein Bashe, Amewataka Maafisa Ugani kutekeleza wajibu wao ipasavyo ikiwemo na kuwatembelea Wakulima katika maeneo wanayolima ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima Mkoani Ruvuma.
Hayo yametamkwa katika mkutano wa wadau wa kilimo Manispaa ya Songea uliofanyika tarehe 16 Januari 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambao ulishirikisha viongozi ngazi ya Mkoa, Wilaya, viongozi wa vyama vya siasa na wadau wa kilimo kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali za wananchi.
Mhe. Bashe, Alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kutoa Mbolea ya Luzuku kwa Mkulima ambayo inauzwa kwa Bei elekezi ya Luzuku iliyopangwa na Serikali kwa lengo la kuwasaidia Wakulima waweze kuondokana na adha ya Mbolea kuuzwa kwa bei ya juu.
Alisema kwa mwaka 2022 Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na Hekta za kilimo 530,000, Tan za Mbolea 32,000, kwa mwaka 2023 Mkoa wa Ruvuma hadi hivi sasa umepokea mbolea Tan 42,000 kwa Hekta za kilimo 930,000.
Amewataka Mameneja wa Makampuni, TFRA, na Mawakala wa Pembejeo kufanya kazi kwa weredi na uadilifu katika kutoa huduma bora kwa wananchi na kuepuka udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara katika usambazaji na uuzaji wa Pembejeo za kilimo na endapo atabainika mtu yeyote anakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa atafutiwa Uwakala. “ alisisitiza”
Aliongeza Serikali imejipanga vizuri katika zoezi la usambazaji wa pembejeo, na amewatoa hofu wakulima wote Nchini juu ya uapatikanaji wa pembejeo kwa kila mkulima aliyesajiliwa lazima atapata pembejeo lakini kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Serikali.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima ndugu Batazari Mjinga Mkulima wa kijiji cha Mhalule alianza kwa kutoa shukrani za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha Mfumo mpya wa kidigiti ambao unawasaidia Wakulima kupata mbolea ya Luzuku 50% ambao ni Mkombozi wa Mkulima.
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa