NAIBU Waziri wa Madini Doto Biteko amefanya ziara katika machimbo ya Ngapa yaliyopo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kuzungumza na wachimbaji wadogo wanaochimba madini ya vito aina ya Gem Stone na kubaini wachimbaji wadogo wananyonywa na wafanyabiashara katika hali inayosikitisha.
Imebainika kuwa baadhi ya wafanyabiashara wananunua madini hayo kwa bei ya chini ambapo wao wanakwenda kuyauza madini hayo mara 15 ya bei walionunulia.Wilaya ya Tunduru haijanufaika na madini tangu mwaka 1996,ambapo kwa mara ya kwanza imepata mapato ya madini katika mwaka 2017/2018 kwa kupata shilingi milioni 66.
Naibu Waziri wa Madini amesema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli baada ya kuona watanzania hawanufaiki katika sekta ya madini imefanya mabadiiko katika sheria ya madini ambapo sasa mtanzania amepata fursa ya kumiliki uchumi katika sekta ya madini.
Mwandishi ni Afisa Habari Serikalini mawasiliano yake ni albano.midelo@gmail.com,simu 078476517
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa