Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Alto Liwolelu amewataka Maafisa Watendaji wa Kata na Mitaa wahakikishe wanafuatilia wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti shule sambamba na ufuatiliaji wa taarifa za wanafunzi waliohama.
Kauli hiyo imetolewa jana tarehe 08 januari 2024 akiwa kwenye zoezila uhakiki wa wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza, awali, darasa la kwanza iliyofanyika katika shule za Sekondari zote, shule za Msingi pamoja na shule mpya 3 ambazo zimesajiliwa na zimeanza kupokea wanafunzi ikiwemo na Chief Zulu Academy, Chief Mbano, na Lawrence Gama kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wawanafunzi walioripo na ambao hawajaripoti shule.
Manispaa ya Songea ina jumla ya shule za Msingi 101 kati ya hizo shule za Serikali ni 84 na Binafsi 17, ambapo kwa upande wa shule za Sekondari jumla ni 43 kati ya hizo shule za Serikali ni 26 na binafsi 17.
Alto alisema” Aliipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha Mil. 560 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya Lawrence Gama Sekondari ambayo imejengwa kwa gharama ya Mil. 560 SEQUIP ambayo imepangiwa wanafunzi 173 kati ya hao wasichana 89 na wavulana 84 na walioripoti ni 30 pia walitembelea Shule ya Msingi Chief Mbano ambayo imejengwa kwa gharama ya Mil. 513 fedha za BOOST . Alipongeza”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa