*Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo.*
#Kila Afisa Habari atoe taarifa ya nini kinaendelea katika Halmashauri yake ili Wananchi wajue nini Serikali inafanya.
#Mikoa na Halmashauri zote nchini zitenge fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya Maafisa Habari, zikiwemo Kamera na Kompyuta ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
#Halmashauri zote zihakikishe Maafisa Habari wanaingia katika vikao vyote muhimu vya Menejimenti ili aweze kuijua Taasisi yake kwa kina.
#Wakuu wa Idara za Mikoa na Halmashauri toeni takwimu kwa Maafisa Habari ili waweze kuweka taarifa hizo kwenye tovuti za Serikali.
*Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Susan Mlawi.*
#Tumesisitiza Wasemaji wa Serikali kuwa mstari wa mbele kutoa habari za Serikali kwa wakati na uhakika.
#Ninaamini mada mbalimbali zilizojadiliwa zimewajengea uwezo na weledi Maafisa Habari katika kuisemea na kuitetea Serikali.
#Mkutano huu umewaongezea ufahamu Maafisa Habari kwa kuwaletea wataalamu waliotoa mada za utekelezaji Serikalini kama vile masuala ya sera ya viwanda, mageuzi katika upatikanaji wa dawa kupitia Bohari ya Dawa (MSD) na maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ( Standard Gauge).
*Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.*
#Maafisa Mawasiliano ni jeshi kubwa linalotegemewa na Serikali katika kutangaza shughuli na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.
#Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itashirikiana na Wizara ya Habari kuhakikisha Maazimio yote yaliyoafikiwa katika mkutano huu yanatekelezwa katika Vitengo vyote vya Mawasiliano vya Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha.
*Imeandaliwa na Idara ya Habari ( MAELEZO).*
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa