Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe.Wilman Kapenjama Ndile amezitaka Asasi za kiraia kuhamasisha shughuli za maendeleo katika jamii ili kuunga mkono jitihada za Serikali.
Asasi za kiraia (NGO’S) ni chombo muhimu ambacho husaidia kutoa huduma na kutatua changamoto katika jamii ikiwemo kutoa elimu ya uzazi wa mpango kwa jamii, mapambano dhidi ya Ukimwi na madawa ya kulevya, mapambano dhidi ya malaria, pamoja na kutoa huduma kwa watoto na wazee waishio mazingira hatarishi na nyinginezo.
Akizungumza na mashirika yasiyo ya serikali (NGO’S) katika mkutano wa mwaka wa fedha 2021/2022 wilaya ya Songea ambao umefanyika Mei 25 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ulio huhudhuriwa na viongozi wa dini, watalaamu pamoja na wadau kutoka asasi mbalimbali kwa lengo la kufanya tathimini ya utendaji wa kazi wa kila mwaka.
Mhe. Ndile amezitaka asasi za kiraia kujisajili katika katika Halmashauri zao kupitia Idara ya maendeleo ya jamii na ofisi ya msajili ya mkuu wa wilaya ya Songea ili ziweze kutambulika kisheria kwa kuzingatia miongozo husika.
Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Songea Martin Mtani ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea kutoa elimu katika jamii juu ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kupinga vikali ndoa ya jinsia moja yakiwa na lengo la kuunga juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita ili kulinda na kuimarisha mila na desturi ya kitanzania.
Aidha jumla ya ASAS za kiraia 37 kiwilaya zimeshiriki kikao hicha ambapo kati ya hizo 15 kutoka Manispaa ya Songea na 22 kutoka halmashauri ya Wilaya ya Songea pamoja na halmashauri ya Madaba.
Akibainisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na utendaji kazi mzuri wa Asasi hizo ikiwemo na kusaidia serikali kukusanya takwimu maalumu kwa ajili ya mipango ya maendeleo, kutoa elimu ya mafunzo ya kilimo pamoja na kuunganisha nguvu ya pamoja kati ya mashirika na serikali katika kuleta maendeleo katika jamii. “Mtani alieleza.”
Wakizungumza na chanzo hiki washiriki wa ASAS hizo walisema “Tunatoa shukrani kwa sekretarieti ya wilaya ya Songea kwa kuanda mkutano huo ambao unatoa miongozo namna ya kutekeleza shughuli mbalimbali kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na serikali ili kuleta maendeleo katika wilaya ya Songea na Taifa kwa ujumla. “walishukuru.”
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa