Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mji Nanyamba Mtwara Jamali Abdalah Kapende amewaongoza Madiwani katika kutembelea Manispaa ya Songea kwa ajili ya kujifunza namna ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 10 Januari 2023 katika Halmashauri Manispaa ya Songea ambapo walifanikiwa kutembelea Miradi mbalimbali ikiwemo Stendi mpya ya Mabasi Songea, Vikundi, Machinjio ya kisasa Songea pamoja na Kituo cha Afya Lilambo kilichojengwa kwa fedha za mapato ya ndani.
Kapende amewataka Madiwani na Wataalam wote kuendelea kutoa ushirikiano katika kukusanya mapato pamoja na kuongeza ubunifu katika kuibua vyanzo mbalimbali vya Mapato ndani ya Halmashauri ili kufikia matarajio ya Serikali yaliyowekwa.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba Deogratius Nsanzugwanko amewataka viongozi na wataalamu kuongeza ushupavu na uimara katika kutekeleza shughuli za Serikali ambazo zitasaidia kuonesha taswira nzuri na kuleta tija ya Maendeleo katika Halmashauri/Nchi kwa ujumla.
Aliogeza kuwa Ziara hiyo imejaa mafanikio kutokana nakujifunza namna ya ukusanyaji wa mapato kwa kuweka wasimamizi kwa kila chanzo cha mapato ( Meneja) hali ambayo imepelekea kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri, pamojaa na namna ya ukopeshaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake 4%, Vijana 4%, na walemavu 2%, Usimamizi bora wa miradi ya maendeleo, na matumizi sahihi ya sheria ndogo za Halmashauri.
Kwa upande wao Madiwani wa Nanyamba Mtwara walisema kupitia Ziara hiyo wamejifunza namna ya uendeshaji wa machinjio ya kisasa, utoaji wa mikopo ya uwekezaji kwa vikundi (uwekezaji wa viwanda vidogo). "walishukuru"
Kwa upande Naibu Meya Jeremiah Milembe alitoa shukrani na kuwakaribisha tena kuja kutembelea kwa mara nyingine kwa ajili ya kufanya tathimini kupitia shughuli walizojifunza ili kubaini mafanikio na changamoto wakati wa utekelezaji na usimamizi wa zoezi la ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo madini, vibali vya sherehe, lessen za vileo, na utoaji wa mikopo kwa vikundi.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa