Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka viongozi wa Chama Cha Akiba na mikopo Manispaa ya Songea - SACCOS kuwa wabunifu wa miradi mingine mikubwa ili kukuza mfuko wa chama.
Akihutubia katika mkutano mkuu wa 30 wa SACCOS Manispaa ya Songea uliofanyika tarehe 29 Oktoba 2022 katika ukumbi wa ST.AUGUSTINE ( AJUCO ) kwa lengo la kutoa taarifa za utekelezaji wa chama uliohudhuriwa na wanachama, mrajisi kutoka ofisi ya Mkoa wa Ruvuma, Kaimu Mratibu wa Programu ( MoCU) pamoja na wakaguzi wa nje kutoka COASCO.
Mhe. Mbano amewapongeza wanachama na viongozi wa chama cha kuweka akiba na mikopo Manispaa ya Songea SACCOS kwa kukikomboa chama kwa kuendelea a kusimamia misingi bora ya uendeshaji wa SACCOS ambayo inasaidia kuinua kipato cha mwanachama ambapo ushirika ni mkombozi wa utendaji wa shughuli za miradi.
Mwenyekiti wa Bodi Amiry Ayoub Khalfani alisema “Chama cha Akiba na Mikopo Manispaa ya Songea “SACCOS” kilianzishwa januari 1988 na kuandikishwa aprili 4, kwa namba RVR 153 na kupewa leseni ya huduma ndogo ya fedha mwaka 2021 ambacho kwa mwaka 2022 walikisia kukusanya fedha za chama 640,000,000 kutoka makusanyo ya ndani ikiwa hali halisi ya makusanyo ni kiasi cha Tsh Mil. 489,827.78 sawa na asilimia 76.50 ya lengo walilojiwekea.”
Amiry aliongeza kuwa kwa mwaka 2022 Chama kilikisia kutoa mikopo ya dharula, elimu, pembejeo, na mikopo ya maendeleo yenye thamani ya 450,000,000 hadi kufikia septemba 30 mikopo iliyotolewa ni 415,700,000 sawa na asilimia 92% kwa jumla ya wanachama 101.
Kwa mujibu sheria ya vyama vya ushirika na masharti ya chama kutochangia akiba ni kinyume na masharti ya chama na 16 (1) (C ) na mwanachama ambaye endapo atakuwa hajachangia akiba kwa zaidi ya miezi 6 kwa mujibu wa masharti ya chama 18 (18) (j) atakuwa amekoma uanachama wake.
Alibainisha kuwa kwa mwaka 2022 chama kiliweka makisio ya mapato ya shilingi 90,500,000 kutokana na faida ya juu ya mikopo, viingilio, na mapato mengine hadi kufikia septemba 30 2022 chama kimekusanya shilingi 57,507,795 sawa na asilimia 64% ya makisio ya mwaka 2022.
Naye makamu mwenyekiti wa bodi Zacharia Kapinga alisema “ hadi kufikia septemba 30 2022 chama kina mtaji ghafi ambao ni akiba za wanachama hisa na akiba za hiari kiasi cha 896,499,946.93 ambazo hutumika kukopesha wanachama kwa masharti na riba nafuu ya asilimia 12 hadi 15 kulingana na mikopo utakaotolewa “
Kapinga aliongeza kuwa miongoni mwa mafanikio yanayopatikana ndani ya chama ni chama kujiendesha chenyewe kwa kutumia mtaji wake wa ndani unaotokana na rasilimali za wanachama ikiwemo na akiba na hisa za hiari, chama kusajiliwa na Baenki kuu ya Tanzania na kupata leseni ya kutoa huduma ndogo za fedha kuanzia tarehe 17 mei 2021, huduma ya mikopo, rambirambi na kufanya shughuli za uendeshaji wa chama,kukodisha jengo lake la kitega uchumi, kutoa mikopo asilimia 92.2% hadi septemba 2022.
Naye Evaristo Benitho kaimu Mratibu wa programu, chuo kikuu wa Ushirika Moshi ( MoCU) Mkoa wa Ruvuma ametoa elimu kwa wanachama wote kwa lengo la kuwajengea uelewa juu ya haki na wajibu kwa mwanachama, viongozi, na kamati tendaji.
Benitho aliongeza kuwa ushirika unaongozwa na misingi saba 7 ambayo ipo kwa utaratibu wa ushirika kidunia ambao umeainisha utoaji wa mafunzo na taarifa kwa viongozi, wanachama na kamati tendaji kwa kuwajengea uelewa wa pamoja katika kutekeleza malengo ya kuandikishwa ili yaweze kutimia kwa mujibu wa kibali chao au leseni yao.
Alibainisha kuwa Wanachama ni sehemu ya wasimamizi na wanufaika wa huduma za chama naniwateja wa chama ambapo wanachama hao hutengeneza kundi jingine kwa maana ya wajumbe wa Bodi ambao endapo wapata mafunzo hayo yatasaidia kuondoa au kupunguza migogoro.
Kwa upande Mrajisi Msaidizi Mkoa wa Ruvuma Peja Moja amewataka viongozi wa chama cha SACCOS kuzingatia sheria ya huduma ndogo za fedha namba 10 ya mwaka 2018 na kanuni zake, kuzingatia miongozo yote waliyopewa na mrajisi, wazingatie tathimini sahihbi za mrejeshaji, pamoja na vikao vya kila robo view na ajenda za kudumu za ukusanyaji wa madeni.
AMINA PILLY.
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa