Maadhimisho siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 16 Juni kwa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika ikiwemo Nchi ya Tanzania ambapo chimbuko la maadhimisho hayo ni baada ya kutokea kwa mauaji ya watoto 2000 yaliyofanywa na Utawala wa Makaburu katika kitongoji cha SOWETO nchini Afrika ya Kusini mnamo tarehe 10 Juni 1970.
Mauaji hayo yalitokea wakati wa maandamano ya wanafunzi kwa lengo la kupinga Mfumo wa Elimu ya kibaguzi iliyokuwa inatolewa na Utawala wa Afrika ya Kusini ambapo 1991 Uongozi wa Nchi za Afrika walifanya uamuzi wa kuienzi siku hiyo ikiwa ni kumbu kumbu ya mauaji ya watoto hao.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Wilaya ya Songea Mhe. Elizabeth Nyembele ambayo yamefanyika kihalmshauri na kuhudhuriwa na viongozi, wadau pamoja na wanafunzi yaliyofanyika katika Uwanja wa Majimaji leo tarehe 16 Juni 2023.
Bi Elizabeth amesema Serikali imeridhia na kusaini Mikataba inayohusu Haki za Watoto (1991) na Mkataba wa Afrika wa Haki ya Ustawi wa Mtoto ya mwaka 2005 ambayo yote kwa pamoja imetoa miongozo ya kusimamia ulinzi na haki kwa mtoto.
Katika kuimarisha ulinzi wa mtoto Manispaa ya Songea kupitia jeshi la polisi imeanzisha dawati la jinsia na watoto katika kituo cha Polisi kwa lengo la kupokea taarifa za matukio ya ukatili dhidi ya watoto na watuhumiwa kuchukuliwa hatua za kishera pamoja na uundaji wa kamati za ulinzi wa mwanamke ngazi ya Wilaya, kata na mitaa kwa lengo kuibua changamoto na namna ya kuzitatua. “Alibainisha”.
“Ametoa wito kwa wazazi au walezi wahakikishe wanawasimamia watoto nakujiepusha kwenda kwenye maeneo ambayo ni hatari kwa usalama, kufuatilia mienendo na kumuepusha mtoto na vitendo vya ukatili ikiwa pamoja ulawiti na mimba, ubakaji, matumizi mabaya ya mitandao na simu, pamoja na kutoa malezi yenye maadili na kutimiza wajibu wa kuheshimu wazazi, walimu na jamii.“
Kwa upande wake Mratibu wa Maadhimisho (Afisa Maendeleo ya Jamii ) Bi Joyce Mwanja alisema “Kauli mbiu ya mwaka 2023 inaelekeza kuweka mazingira Salama na kuchukua tahadhari dhidi ya watoto wanapokuwa mitandaoni ambayo inaikumbusha jamii pamoja na wazazi kutumia matumizi sahihi na salama dhidi ya vifaa vya kieletroniki na intanenti kutokana na uwepo wa vitendo vingi vya ukatili vinavyofanyika mitandaoni ikiwemo na simu.
Bi Joyce aliongeza kuwa kauli mbiu hiyo imelenga kuhamasisha Serikali, Wananchi, Taasis, Asasi, wadau mbalimbali kushiriki kikamilifu katika suala la malezi, makuzi, ulinzi na maendeleo ya mtoto.
KAULI MBIU; ZINGATIA USALAMA WA MTOTO KATIKA ULIMWENGU WA KIDIGITALI.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa