Siku ya wazee Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 01 Oktoba ya kila mwaka kwa ajili ya kukumbushana umuhimu wa wazee ili waweze kuwa na maisha bora yenye kuleta matumaini aidha wanapokuwa wamestaafu au wanapokuwa na umri mkubwa.
Katika kutekeleza maadhimisho hayo Halmshauri ya Manispaa ya Songea ilifanikiwa kuandaa maadhimisho yaliyofanyika katika uwanja wa majimaji na kuhudhuriwa na wananchi pamoja na wadau wa wazee kwa lengo la kukuza ustawi wa wazee na kuondoa ubaguzi dhidi yao.
Mgeni rasmi katika maaadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye aliwakilkishwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema ambaye alianza kwa kusema “ Ni wajibu wa kila mwanajamii katika kuwalinda na kuwathamini wazee ambao ni kundi muhimu katika jamii ambapo wanahitaji kulindwa na kuheshimiwa.”
Pololet aliongeza kuwa malengo makubwa ya Sera ni kuhikikisha kuwa wazee wanathaminiwa na kutunzwa na jamii na kushirikishwa katika shughuli za kijamii kwa maendeleo ya Taifa letu pamoja na kuwapatia huduma bora za afya hususani katika vituo vya afya, Zahanati, Hasptali, na kuahakikisha wanapewa haki kwa wazee kabla ya wengine.
Alisema Serikali ipo kwenye hatua mbalimbali za kuhakikisha wazee wote wanawekwa kwenye Mfumo wa malipo ya Pensheni pamoja kutunga sheria ya haki za wazee na kuhakikisha yanaundwa mabaraza ya wazee kila Mkoa ambayo yanasaidia kuwaunganisha wazee
Alitoa agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa Ruvuma kuhakikisha anasimamia na kuboresha kuhusu upatikanaji wa dawa kwa wazee ambao ni hazina kwa Taifa, pamoja na kuhakisha inatengwa bajeti kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani.
Ikisomwa Risala kutoka baraza huru la wazee ambayo walisema “ Maadhimisho ya siku ya wazee duniani ni utekelezaji wa azimio la umoja wa Mataifa namba 45/106/1990 kwalengo la kuelimisha, kujenga amasa na uelewa katika kuboresha naman ya upatikanaji wa huduma bora na ustawi wa wazee katika jamii.
Kauli mbiu ya mwaka 2022 ni “USTAHIMILIVU NA MICHANGO YA WAZEE NI MUHIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA.”
Na;
AMINA PILLY
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa