NA,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
01.10.2021
Manispaa ya Songea yaungana na Mataifa mengine duniani kusheherekea maadhimisho ya siku ya Wazee duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 1 ya mwezi wa kumi.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Zimanimoto uliopo katika Manispaa ya Songea na kuudhuriwa na viongozi pamoja na wananchi ndani ya Manispaa ya Songea ambapo Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Ibuge alianza kwa kuwapongeza wazee wote waliojitokeza kusheherekea siku yao na kuwahakikishia changamoto zote waliozozieleza zinafanyiwa kazi ambapo miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na wazee kuendelea kupewa kipaumbele kwenye kupata huduma za afya bure hasa upatikanaji wa dawa ambao umekuwa ukisumbua kwa muda mrefu.
Ibuge amewataka maafisa maendeleo ya jamii kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wazee kwa kuandaa siku maalumu kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi na kuzifanyia kazi pamoja na kuhakikisha wanapata haki zao stahiki.
Amesema kuwa kilio cha wazee na wakulima Mkoa wa Ruvuma ni upandishwaji wa bei za pembejeo za kilimo hasa mbolea hali iliyosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa UVIKO 19 ambapo viwanda vyaa uzalishaji mbolea duniani ulisimama na hivyo kupelekea uhaba wa mbolea na kupanda kwa bei ya pembejeo hiyo.’Alibainisha’
Ibuge amewatoa hofu wazee na wakulima kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha bei ya pembejeo za kilimo zinakuwa rafiki na nafuu kwa wananchi wake kwa kupanua soko ambapo mtu yeyote anaruhusiwa kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi endapo atafuata utaratibu uliowekwa na kwa kufanya hivyo uapatikanaji wa mbolea hiyo utaongezeaka na hivyo kupunguza gharama za ununuzi wa pembejeo hiyo.
Alihitimisha kwa kuwahamasisha wazee wote Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa manufaa ya afya zao pamoja na kushiriki kikamilifu kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi kitaifa inayotarajiwa kuanza kufanyika mwaka 2022.
Kwa upande wake katibu wa baraza huru la wazee Yohana Mbalale alisema kuwa siku hii ya wazee duniani ilitengwa rasmi na baraza la Umoja wa Mataifa kupitia azimio No 45/106 la mwaka 1920 kwa lengo la kuelimisha , kuleta hamasa na uelewa katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora na haki za wazee katika jamii waliyopo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wazee duniani kwa mwaka 2021 ni;
“MATUMIZI SAHIHI YA KIDIGITALI KWA USTAWI WA RIKA ZOTE”.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa