Halmashauri ya Manispaa ya Songea imekuwa ikiendelea kuendesha zoezi la usafi wa mazingira wa mwisho wa mwezi uliofanyika tarehe 26 Novemba 2022 katika maeneo mbalimbali ndani ya mji.
Afisa mazingira Manispaa ya Songea Beno Philipo amewataka wananchi wote kufanya usafi katika maeneo wanayoishi pamoja na maeneo mbalimbali wanayofanyia shughuli ambapo kwa mwezi Novemba zoezi la usafi wa pamoja limefanyika katika eneo la soko kuu lililopo kata ya mjini.
Alisema zoezi hilo litakuwa endelevu na litakuwa ikifanyika kila ifikapo tarehe ya mwisho wa mwezi ili kuweka mji safi.
Kwa upande wa wananchi walioshiriki usafi wamazingira walisema " wameipongeza Serikali kwa kuanzisha zoezi hilo na wameomba Serikali kuchukua hatua kwa yeyote atakaye kiuka zoezi hilo." Walipongeza"
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa