Katibu Tawala Wilaya ya Songea Pendo Daniel amezindua zoezi la umezaji wa dawa tiba na kinga dhidi ya magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ambalo hufanyika kuanzia tarehe 22 septemba hadi 24 septemba 2022 kwa kufanya sensa na kugwa dawa kwa lengo la kudhibiti dhidi ya magonjwa ya mabusha, Matende, Minyoo, na kichocho.
Akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake Bi pendo alisema kuwa ugonjwa wa USUBI ni ugonjwa unaoenezwa na minyoo inayoitwa “ONCHOCERCA VOLVULUS” ni minyoo inayonezwa na inzi weusi wadogo wanaokaa kando kando ya mito ya maji yaendayo kwa kasi ambao husababisha ngozi kuwasha au kuwa na mabakamabaka meusi mithili ya mamba au mjusi mweusi.
Alisema zoezi hilo la umezaji wa dawa za USUBI linafanyika katika Halmashauri zote 8 Mkoani Ruvuma ambapo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea zoezi litafanyika kwa siku 3 ambapo limeambatana na zoezi la semina elekezi kwa Wenyeviti wa mitaa 95, Watendaji wa kata 21, na wahudumu wa afya.
Ametoa rai kwa wananchi wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kujitokeza kwa wingi na kuhakikisha wanameza dawa hizo ambazo hazina madhara yoyote bali ni kinga ya upofu mto.
Kwa upande wake Mratibu wa Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele Manispaa ya Songea Bload Komba alisema “Uzindunduzi wa unyweshaji dawa kwa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa wananchi 252282 ambao matarajio ni kwa watu wasiopungua 201,830 sawa na asilimia 80% na watu ambao hawataruhusiwa kumeza dawa za usubi ni kwa watoto walio chini ya miaka 5, wamama wajawazito, na wagonjwa mahututi. Alibaisha.
Bload amewatoa hofu wananchi wote kuwa dawa za USUBI ni salama hazina madhara yoyote hata hivyo dawa hizo hutolewa kila mwaka kwa ajili ya kutibu na kudhibiti wa USUBI kwa kumeza dawa aina ya MECTZAN Kwa miaka kumi mfululizo.
Kwa upande wa wananchi Wakitoa ushuhuda mara baada ya kumeza dawa za Usubi ambapo walisema kuwa dawa za usubi hazina madhara yoyote na wametoa rai kwa wananchi kuondoa hofu juu ya dawa za USUBI na kuthibitisha kuwa zinasaidia kuepukana na mangonjwa ya ngozi.
Imeandaliwa na;
AMINA PILLY.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa