Manispaa ya Songea imeendesha Bonanza la michezo kwa ajili ya kuwaaga watumishi waliostaafu 25, watumishi wa ajira mpya 67 na kuukaribisha mwaka 2023 iliyoambatana na tafrija fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Bombambili.
Bonanza hilo lilifanyika tarehe 07 Januari 2023 katika uwanja wa Majimaji ambapo kulikuwa na michezo mbalimbali ambayo ilichezwa ikiwemo na mpira wa Simba na Yanga, mchezo wa kukimbiza kuku, kula Mkate, Kukimbia na kijiko cha yai, kukimbia na Magunia na mchezo wa kuvutana kamba.
Dkt. Frederick Sagamiko amewataka watumishi wake wote kutenga muda wa kufanya mazoezi ya viungo vya mwili ili kujenga afya ya mwili na akili ambapo ametoa rai kushiriki bonanza la michezo ifikapo wiki ya mwanzo ya mwezi April 2023.
Akizungumza na watumishi wastaafu katika ukumbi wa Bombambili wakati anatoa zawadi ya vyeti kwa wastaafu hao ambapo alisema “Nidhamu na uadilifu katika utumishi umewsaidia kufikia hatua ya kustaafu hivyo amewataka wastaafu kutenga muda wa kupumzika na kuepukana kufanya kazi ngumu ambazo zinaweza kuathiri afya zenu “ aliwapongeza.”
Naye Meneja wa CRDB Songea Method Muganyizi aliunga mkono Bonanza hilo kwa kutoa vinywaji baridi pia alimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea kwa kuandaa na kutenga muda wa kuandaa tafrija la kuwaaga watumishi wastaafu na kuwakaribisha watumishi wa ajira mpya, "Muganyizi alipongeza"
Imeandaliwa na ;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa