Waziri wa Katiba na Sheria (MB) Dkt.Damas Ndumbaro amewataka wananchi wa Manispaa ya Songea kuunda vikundi vya wajasiliamali wadogo kwa ajili ya kupata mikopo ya 10% kupitia vikundi vya wanawake 4%, vijana 4%, na walemavu 2% ili kuinua kipato cha jamii.
Hayo yamejili katika ziara ya Mbunge wa jimbo la Songea Mjini iliyofanyika kwa siku 5 kuanzia tarehe 30 Novemba hadi 4 Desemba 2022 na kufanikiwa kutembelea kata 9 ambazo ni kata ya Bombambili, Matarawe, Mletele, Mateka, Matogoro, Seedfarm, Msamala, Ruhuwiko na Lizaboni.
DKT. Ndumbaro (MB) amesema katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2022 Serikali imetekeleza na kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo na ujenzi wa vyumba vya madarasa fedha za UVIKO 19, ujenzi wa vituo vya afya vipya vitano 5 na Hospitali ya Wilaya 1 pamoja na Hosptali ya Rufaa ya Mkoa 1 iliyopo Mwengemshindo, kujenga Chuo kikuu kipya cha Uhasibu Arusha, Masoko mawili ya kisasa (Manzese), ujenzi wa uwanja wa ndege, daraja ya Matarawe- Mjiwema, Mikopo kwa vikundi bil. 1 kwa mwaka, Barabara kutoka Sanga one hadi Tanroad, kujenga barabara ya kiwango cha Lami km 13 katika kata ya Mfaranyaki, Misufini, na Majengo na miradi mingineyo.
Aliongeza kuwa lengo la kufanya mikutano ya hadhara katika kata ililenga kupokea chanagamoto za kutoka kwa wananchi ambazo zimekuwa kero katika jamii ambapo kupitia mikutano hiyo aliweza kupokea baaadhi ya kero ambazo amehaidi kuzitafutia ufumbuzi na pamoja na ukarabati wa miundombinu chakavu ya madarasa, barabara za mitaa, maji kwa baadhi ya kata, uhitaji wa vituo vya afya katika kata ya Bombambili, Ruhuwiko, na Lizaboni, uhitaji wa shule za Sekondari mpya kwa kata ambazo hazina Sekondari za kata kama Seedfarm, Ruhuwiko na Ndilima Litembo.
Akitoa ufafanuzi juu ya utatuzi wa changamoto Mikopo “ alisema Manispaa ya Songea imeendelea kutoa mikopo ya asilimia 10% kwa kutenga fedha kila robo ya mwaka ambapo kuanzia Julai hadi Septemba imetenga kiasi cha shilingi Mil. 215 kwa ajili ya vikundi ambapo hadi hivi sasa mikopo hiyo haijatolewa kutokana na kukosa wakopaji wenye sifa.
Akijibu changamoto ya baadhi ya kata ambazo zina uhitaji wa kituo cha afya na sekondari mpya alisema Serikali imeweka mpango wa kujenga vituo vya afya vine vipya katika kata ambazo zina sifa ya kupata vituo hivyo pamoja na ujenzi wa shule za Sekondari mpya tatu kwa lengo la kuondoa kabisa tatizo la mlundikano wa wananfunzi madarasani.
Manispaa ya Songea ipo katika hatua za kuanza utekelezaji wa mradi wa maji kwa ambapo Serikali imeshasaini mkataba wa utekelezaji wa mradi huo kwa nchi zima katika miji 28 kati ya miji hiyo Songea ikiwemo ambapo utaratibu wake utatatolewa hivi karibuni.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt, Frederick Sagamiko alisema changamoto ya barabara za mitaa haita kuwepo kwa sasa kwani Manispaa imeandaa utaratibu kupitia TARURA wa kutatua chanagamoto hizo ambapo ameagiza kata zote 21 kuleta taarifa zenye ufafanuzi wa maalum wa mahitaji ya miundombinu korofi ambayo inahitaji kutekelezwa ikiwemo na barabara za mitaa, vivuko vyote, madaraja, na mifereji ili TARURA waweze kutekeleza .
Aliongeza kuwa Manispaa ya Songea inatarajia kuanza kujenga Chuo Kikuu katika mtaa (Pambazuko) ambacho kitatoa masomo ya Biashara na Uhasibu ambapo serikali imetenga shilingi Bil.17 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo ambao ulikuwa ni moja ya kilio na deni kubwa kutoka kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Akitolea ufafanuzi juu ya Ujenzi wa Masoko 2 ya kisasa(Manzese) alisema kuwa Serikali inatarajia kutangaza kazi ya ujenzi wa masoko mawili 2 ambapo zoezi linatarjia kufanyika mwezi Disemba kwa ajili ya kupata Mkandarasi ambaye atakuwa fundi wa kujenga masoko ambapo ujenzi huo utaambana na ujenzi wa utengenezaji wa barabara KM 13.
Naye Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amesema Manispaa imetenga bajeti ya shilingi Mil. 20 kupeleka kila kata ambazo zitasaidia kutatua chanagmoto ya mbalimbali za kata husika ikiwemo ukarabati wa miundombinu ya madarasa chakavu.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa