MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas amewataka viongozi na wataalamu wa Manispaa ya Songea kukamilisha miradi ya ujenzi kwa wakati muafaka ili iweze kutumiwa na wananchi.
Hayo yamejili katika ziara ya Mkuu Mkoa wa Ruvuma iliyofanyika tarehe 28 Novemba 2022 na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kukagua hatua ya miradi na kisha kuzungumza na watumishi wa Manispaa ya Songea.
Ziara hiyo imefanyika kwa siku moja ambapo aliweza kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Lilambo kinachojengwa kwa fedha za mapato ya ndani Mil. 514, ujenzi wa vyumba vya madarasa 6 katika shule ya chandarua sekondari fedha kutoka serikali kuu Mil. 120, Ujenzi wa vyumba vya madarasa 6 Lizaboni sekondari fedha kutoka Serikali kuu Mil. 120, kituo cha afya fedha kutoka Grobal Fund Mil.545, pamoja na ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Matogoro kwa fedha kutoka Serikali kuu Mil. 40.
Kanal Laban alianza kwa kuwapongeza Manispaa ya Songea kwa kufanikisha kujenga ujenzi wa kituo cha afya kilichopo kata ya Lilambo kilichojengwa kwa gharama ya Mil. 514 fedha kutoka mapato ya ndani ambapo ujenzi wake upo hatua ya ukamilishaji.
Amewataka wataalamu hao kushirikisha wananchi kila wanapotekeleza mradi kwenye kata husika ili kuleta uwazi na ushirikishwaji jamii ambao utaleta ulinzi shirikishi katika kulinda rasilimali za umma ikiwemo kuundwa kwa kamati za ujenzi ambazo zinajumuisha wanajamii.
Ametoa agizo kwa viongozi ngazi ya Wilaya na Halmashauri kuwa na tabia ya kufanya ziara ya kutembelea miradi mingine inayotekelezwa ambayo sio miradi ya UVIKO au ya ujenzi wa madarasa iliyoanza kujengwa hivi karibuni ili kuleta msukumo wa kiutendaji na kukamilisha kwa wakati.
Aidha, baada ya kukamilisha ziara hiyo, kiongozi alizungumza na watumishi wote wa Manispaa ya Songea ambapo aliwataka watumishi hao kusimamia miradi ya maendeleo kwa usahihi ili kutimiza wajibu na majukumu ya kazi kama mtumishi wa umma.
Ametoa Rai kwa idara ya Usafi wa Mazingira kutumia sheria ndogo za usafi wa mazingira kwa watakao kiuka sheria za usafi wa mazingira ili kuweka mji safi pamoja na upandaji wa miti kwa kila kaya ili kulinda miti ya awali ambayo ipo ndani ya mji.
Akizungumzia kuhusu mahusiano kwa watumishi mahala pa kazi ambapo aliwataka wakuu Idara na Vitengo kujenga mahusiano mazuri baina ya watumishi ambao ni wakuu wa idara na watumishi wa chini yake ili kujenga uhusiana na uwajibikaji bora. “Kanal Laban amesisitiza".
Kanal. Laban amekemea vikali tabia ya baadhi ya watumishi ambao hukiuka taratibu za kiutumishi wa umma ambapo alitamka nanukuu” ukipata ajira sio umepata utajiri na ukitafuta utajiri wakati ni mtumishi wa umma unatafuta kutenda vitendo ambavyo sio sahihi katika utendaji wa Serikali.” Mwisho wa kunukuu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Kamando Mgema alisema “ watumishi ndio injini ya maendeleo ya Halmashauri na kila mmoja akitekeleza majukumu yake kupitia idara husika kutakuwa na maendeleo yenye tija, na endapo hatatekeleza kwa umakini hakutakuwa na maendeleo, hivyo amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa weledi na kulinda maadili ya utumishi wa umma.
Naye Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Songea Alto Liwolelu alisema Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwa kipindi cha mwezi Julai hadi October imepokea jumla ya Tshs 2,757,250,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya Elimu, Afya, Maendeleo ya Jamii na Utawala.
Imeandaliwa na;
AMINA PLYY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa