MSTAHIKI Meya Manispaa ya Songea Michael ametoa shukrani kwa Serikali ya awamu ya sita kwa kulipa fidia ya Bil.3.7 kwa wananchi 878 kati ya Wananchi 868 ikiwa ni asilimia 97% na uhakiki unaendelea kwa wananchi 77.
Mstahiki Meya ametamka hayo akiwa katika baraza la madiwani lililofanyika tarehe 23 Agosti 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambalo walishiriki Waheshimiwa Madiwani, Wataalamu pamoja na wananchi kwa lengo la kupokea taarifa za mwaka mpya wa fedha 2023/2024.
Kikao hicho kilianza kwa kupokea maswali ya papo kwa papo kutoka kwa Waheshimiwa madiwani ambayo yalihusu mipango Miji kufuatilia suala la mwananchi kujenga uzio ambao umepelekea kufunga njia ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi wa kata ya Mjini .
Akitoa ufafanuzi Mhe. Mbano, amemtaka Mkurugenzi Manispaa ya Songea kuitisha kikao maalumu cha kamati ya Mipango Miji kwa ajili ya kujadili changamoto hiyo ili wananchi waweze kutumia njia hiyo kama mipaka inavyoonesha katika Ramani ya mipango Mji.
Akizungumza Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro (MB), alianza kwa kutoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuanza kulipa fidia kiasi cha fedha Bil. 5.3 kwa wananchi 955 wa Kata ya Mwengemshindo ambapo kati ya 878 tayari wameshalipwa kwa thamani ya Bil. 3.7.
Dkt. Ndumbaro amewataka Madiwani wote kujipanga katika mchakato wa katiba mpya ambo unakuja ili kutafuta namna bora ya kushirikisha wananchi na sauti za wananchi zisikike kwasababu inahitajika katiba mpya ambayo itaweza kusaidia kwa miaka ijayo.
Alisema Katiba mpya ni Mkataba wa makubaliano kati ya wananchi kwa pande mbili 2 ambao upande mmoja ni wananchi ambao ndiyo wenye mamlaka pia kwa upande wa pili ni watalamu pamoja na vyama vya siasa ambapo inaonesha wanachi kuwa na uhitaji mkubwa wa Katiba mpya.” Alibainisha”
Imeandaliwa na
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa