Naibu Meya Manispaa ya Songea Jeremiah Mlembe amewataka wataalamu kutoa taarifa za vikao vya baraza mapema kwa kupitia Vishikwambi walivyopewa ili waweze kupitia taarifa hizo na kufahamu namna ya kujadili agenda mbalimbali zilizoandaliwa katika baraza hilo.
Hayo yametamkwa kupitia baraza la Madiwani Manispaa ya Songea liliofanyika leo 21 februari 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambalo lilihudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, Wadau mbalimbali pamoja na Mhe. Mbunge wa Viti Maalum Bi Mariamu Nyoka.
Aidha, amewataka wataalamu hao kuandaa ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo ikiwemo na shule ya Chief Zulu iliyojengwa kwa fedha za mapato ya ndani kiasi cha Mil 500 ambayo imeanza kutumika, pia pamoja na mradi wa kikundi cha kiwanda cha Vifungashio kilichopo kata ya Lilambo kilichojengwa kwa fedha za mkopo wa 10%.
Akizungumza Mheshimiwa Mbunge wa Viti wa Maalumu Bi Mariamu Nyoka ambapo ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Songea ikiwemo na ujenzi wa vituo vya Afya, Zahanati, Madarasa, pamoja na miundombinu ya Barabara. "Alipongeza".
Kwa upande wake katibu wa CCM Komredi James Mgego amewapongeza wataalamu wote wa Manispaa ya Songea kwa utendaji wao wa kazi pia amewataka kuandaa taarifa kwa usahihi na kuzituma kwa madiwani kwa wakati ili waweze kupitia na kujadili katika kikao cha mkutano wa baraza husika.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY,
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa