Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano amewataka viongozi na wataalamu kuongeza ufanisi na weredi wa kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato ili kufikia lengo la makisio ya Bajeti iliyowekwa kwa mwaka 2023/2024
Hayo yamejili wakati wa Baraza la Madiwani la kupitisha mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2023/2024 lililofanyika tarehe 09 Februari 2023 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea lililohudhuriwa na wadau mbalimbali, wakuu wa Idara na wananchi.
Mhe. Mbano Alisema Nanukuu “ili kufanikiwa lazima kuongeze juhudi ya kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na wataalamu ili kufanikiwa lengo la makusanyo ya Bil. 5.6 kwa mwaka 2023/2024 ”Mwisho wa kunukuu"
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt. Frederick Sagamiko alisema kuwa mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024 iliyopitishwa itsaidia na kurahisisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali ya maendeleo.
Aidha, matarajio ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea ni kukusanya na kutumia Tsh Bil. 11.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbai ya maendeleo kutoka vyanzo mbalimbali kati ya fedha hizo kiasi cha Bil. 4,6 kutoka Serikali kuu, Waisani Bil. 5.3 na Halmashauri itachangia kutokana na mapato ya ndani kiasi cha Bil. 1.7 sawa na asilimia 40%.
Aliongeza kuwa, Manispaa ya Songea imeomba kuidhinishiwa kiasi cha Tsh Bil. 45.7 kwa ajili ya shughuli ya utekelezaji ambapo kati ya fedha hizo Bil. 30.2 Mishahara na Mil. 98.5 mengineyo, Luzuku ya Maendeleo kutoka Serikali kuu Bil. 8.9, mapato ya ndani yanakisiwa Bil. 5.6 ambapo Bil. 34.4 iliombwa kuidhinishwa kati ya fedha hizo kiasi cha Bil. 31.1 Mishahara na Bil. 3.2 mengineyo.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini Ndg. James Mgego amewataka viongozi na wataalamu kuongeza uwajibikaji, uadilifu katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali pamoja na kufanya ufuatiliaji wa bajeti iliyowekwa iweze kutatua changamoto za wananchi.(Alisisitiza)
Nao Waheshimiwa Madiwani walitoa pongezi zao kwa Wataalamu kwa kutenga bajeti ambayo imegusa kila sekta ambapo ni matarajio yao kuwa Rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 itasaidia kutatua changamoto za wananchi.(Walipongeza)
Imetolewa na;
AMINA PILLY
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa