Kamati ya Lishe Manispaa ya Songea ikiongozwa na Dkt. Frederick Sagamiko ambaye ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, wamefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa Lishe katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2023 kilichofanyika tarehe 20 Oktoba 2023 kwa lengo la kufanya tathimini ya hali ya Lishe kwa watoto chini ya miaka 5 na wamama wajawazito.
Akizungumza Afisa Lishe Manispaa ya Songea Frorentine Kissaka alisema “Katika kupambana na udumavu pamoja na utapiamlo, kitengo kimefanya uchunguzi wa hali ya Lishe kwa kutumia mzingo wa mkono kwa watoto chini ya miaka mitano pamoja na kupima uzito kulingana na umri wa mtoto.
Aidha, ulitolewa unasihi wa Lishe bora kwa akina mama wajawazito, wanaonyonyesha, walezi wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambapo Jumla ya Watoto 37,818 wenye umri wa chini ya miaka mitano walichunguzwa hali ya lishe kati ya 32,216 sawa na asilimia 117%, Kati yao 26 waligundulika kuwa na utapiamlo mkali ambao ni sawa na asilimia 0.07%, Watoto 791 ambao ni sawa na asilimia 2.09% waliochunguzwa waligundulika kuwa na utapiamlo wa kadiri, Watoto 37001 waliochunguzwa sawa na asilimia 97.84% hawakuwa na utapiamlo.
Kissaka alisema katika kutatua changamoto hizo, watoto wote waliongundulika kuwa na utapiamlo wa kadiri walipewa unasihi wa uandaaji wa chakula na ulaji unaofaa lakini waliokua na utapiamlo mkali walipewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa Songea kwa matibabu ya utapiamlo.
Miongoni mwa mikakati iliyowekwa katika kukabiliana na utapiamlo ni pamoja na kila shule kuhakikisha inaongeza idadi za klabu za Lishe kuanzia 20 hadi 50, pamoja na kufanya ufuatiliaji wa bidhaa zilizoongezewa virutubisho (Unga na mafuta).
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa