Kiwango cha maambukizi ya VVU miongoni mwa wanawake kimepungua kutoka asilimia 4.9 mwaka 2015 hadi asilimia 2.9 kwa wanaume kutoka asilimia 4.6 mwaka 2015 hadi asilimia 2.3 mwaka 2018.
Hayo yamebainishwa katika kikao cha robo ya kwanza ya mwaka 2023/24 cha kamati ya kitaifa ya kudhibiti vvu, ukimwi na MSY mahali pa kazi katika utumishi wa umma kilichofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Songea tarehe 23 Oktoba 2023 kwa lengo la kufanya tathimini ya utekelezaji wa Muongozo katika Wizara na Taasis mbalimbali.
Akizungumza mwakilishi wa katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bi. Leila Mavika alisema “ Magonjwa yasiyoambukiza yanaendelea kuongezeka hapa nchini ambapo Ugonjwa wa Shinikizo la Juu la Damu unaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi ambao Takwimu zinaonesha kwa mwaka 2017 kulikuwa na wagonjwa 688,901 na hadi kufikia mwaka 2022 kulikuwa na wagonjwa 1,456,881 sawa na ongezeka la zaidi ya mara mbili katika kipindi cha miaka mitano.
Bi. Leila aliongeza kuwa ” changamoto ya afya ya akili imeendelea kuongezeka hapa nchini ambapo taarifa ya Wizara ya Afya inaonesha kwamba kwa mwaka 2022 jumla ya watanzania 854,154 walipata huduma za matibabu ya Afya ya Akili katika vituo mbalimbali vya Afya.
Katika kutekeleza muongozo, Serikali imeweka malengo mahususi ili kufanikisha utekelezaji wa afua hiyo ikiwemo na Kutenga fedha za kuwezesha utekelezaji wa Mwongozo na Waraka wake kila mwaka, Kujenga uelewa kwa Watumishi wote wa Umma waliopo katika Mamlaka zenu kuhusu Mwongozo pamoja na Waraka wake ili kupunguza hali ya unyanyapaa na kuhamasisha watumishi kujiweka wazi.
Kutekeleza afua zenye lengo la kuimarisha afya na Ustawi wa Watumishi mahali pa Kazi ikiwemo kuhamasisha watumishi kufanya mazoezi kwa kutenga muda maalum wa kufanya mazoezi angalau mara moja kila wiki, Kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza afua mahsusi za kuimarisha Afya ya Akili, Msaada wa Kisaikolojia na Kijamii ikiwa ni jitihada za kuimarisha afya ya akili miongoni mwa Watumishi wa Umma.
Aidha, kuendelea Kutenga fedha kwa ajili ya mafunzo kwa watumishi yenye lengo la kukuza uelewa wa masuala ya udhibiti wa magonjwa hasa elimu juu ya lishe yenye afya, Wizara kuhakikisha zinasimamia taasisi zilizo chini yao katika utekelezaji wa Mwongozo na uwasilishaji wa taarifa,
Kutekeleza afua zenye lengo la kuimarisha afya na Ustawi wa Watumishi mahali pa Kazi ikiwemo kuhamasisha watumishi kufanya mazoezi kwa kutenga muda maalum wa kufanya mazoezi angalau mara moja kila wiki, Kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza afua mahsusi za kuimarisha Afya ya Akili, Msaada wa Kisaikolojia na Kijamii ikiwa ni jitihada za kuimarisha afya ya akili miongoni mwa Watumishi wa Umma.
Aidha, kuendelea Kutenga fedha kwa ajili ya mafunzo kwa watumishi yenye lengo la kukuza uelewa wa masuala ya udhibiti wa magonjwa hasa elimu juu ya lishe yenye afya, Wizara kuhakikisha zinasimamia taasisi zilizo chini yao katika utekelezaji wa Mwongozo na uwasilishaji wa taarifa.
Pia Sekretarieti za Mikoa kuhakikisha zinasimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Utekelezaji wa Mwongozo na uwasilishaji wa taarifa, Kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa afua za kudhibiti VVU, UKIMWI na magonjwa yasiyoambukizwa kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa