Katika kupambana na udumavu pamoja na utapiamlo, Halmashauri ya Manispaa ya Songea kupitia kitengo cha Lishe kimefanya uchunguzi wa hali ya Lishe kutumia mzingo wa mkono kwa watoto chini ya miaka mitano, pamoja na upimaji wa uzito kulingana na umri wa mtoto, katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2023/2024.
Pamoja na uchunguzi huo, kitengo cha Lishe kimetoa unasihi wa lishe bora kwa akina mama Wajawazito ni 2472 kati ya 2472 waliofikiwa sawa na asilimia 100, akina mama Walionyonyesha maziwa ya mama pekee ndani ya saa moja baada ya kujifua ni 2363 kati ya 2434 sawa na asilimia 97, pamoja na akina mama wenye watoto chini ya miaka miwili waliopata unasihi wa ulishaji wa watoto wachanga na wadogo kutoka kwa watoa huduma za Afya 32723 kati ya 33032 sawa na asilimia 99.1.
Hayo yamejiri wakati wa kikao cha kamati ya Lishe Manispaa ya Songea kilichofanyika tarehe 06 Agosti 2024 kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli za lishe katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2023/2024 ambacho kilihudhuriwa na wakuu wa idara ya Elimu Msingi na Sekondari, kilimo, Maendeleo ya jamii, Mipango, fedha na Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe.
Akizungumza Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea ambaye aliwakilishwa na Afisa Mazingira Manispaa ya Songea Beno Mpwessa alisema “katika uchunguzi na unasihi uliofanyika katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2023/2024 kitengo cha lishe kilibaini hali ya lishe lengo ni 32,216 kati yao 37,488 sawa na asilimia 113 walifikiwa, kati ya hao watoto 37,395 sawa na 99.77 hawakuwa na utapiamlo ambapo watoto 10 sawa na asilimia 0.03 waligundulika kuwa na utapiamlo mkali”
Kwa upande wake afisa lishe Manispaa ya Songea Florentine Kissaka alibainisha kuwa, watoto wote walioguindulika kuwa na utapiamlo mkali walipewa rufaa ya kwenda hospitali ya rufaa Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya matibabu ya utapiamlo mkali.ambapo kati ya hao 10 walipatiwa matibabu na watoto 9 walipona na 1 alibaki na hatua za matibabu zinaendelea.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa