Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka Wazabuni kuongeza uwaminifu katika ukusanyaji wa Ushuru wa Mazao pamoja na ukusanyaji wa ushuru wa ada ya usafi wa taka ngumu na kufikia lengo lililokusudiwa katika ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri.
Katika kutekeleza jukumu hilo Manispaa ya Songea imesaini Mkataba na Wazabuni na watoa huduma mbalimbali wakiwemo na WOFMAIZE COMPANY LIMITED kwa ajili ya zabuni ya ukusanyaji wa Ushuru wa Mazao wenye thamani ya zadi ya Bil. 1, MAHOKA TRADING AND SERVICES INVESTIMENT Kwa ajili ya kufanya usafi, kukusanya taka ngumu kwenye makazi ya watu, majengo ya Biashara, Masoko, Stendi za Mabasi, Mitaa na Ofisi mbalimbali na kuzipeleka Dampo la Subira na kukusanya ada za uzoaji taka katika kaya zote za Mjini, Majengo, na Mfaranyaki wenye thamani ya zaidi ya Mil 100.
Wazabuni wengine ni pamoja na NAMALA II CLEANING SERVICES Kwa ajili ya kufanya na kukusanya taka ngumu kwenye makazi ya watu, kwenye majengo ya biashara, Masoko, Stendi za Mabasi Mitaa na ofisi mbalimbali na kuzipeleka Dampo pamoja na kukusanya ada ya uzoaji wa taka katika katika kaya zote za Misufini, Matarawe, na Bombambili wenye thamani ya Mil. 78, pamoja na ASA SECURITY LIMITED ambao watafanya kazi ya utoaji wa Huduma ya Ulinzi.
Hafla hiyo imefanyika leo 28 Julai 2023 ofisini kwake Mstahiki Meya ambayo ilihudhuriwa na Wazabuni mbalimbali,pamoja na Wataalamu kwa lengo la kuingia Mkataba na Wazabuni na watoa huduma.
Mhe. Mbano alisema ‘ Zabani za ukusanyaji wa huduma ya kuzoa taka zilitangazwa kupitia TOVUTI ya Halmashauri, Mbao za matangazo ambapo ilipelea wazabuni hao kushinda Zabuni na hatimaye kusaini Mkataba wa utoaji wa uduma katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.’Aliwapongeza.
Aliongeza kuwa moja ya vigezo vya Halmashauri ni pamoja na ukusanyaji wa mapato pia kiashiria kikubwa cha ukuaji wa mji ni ongezeko la taka maana yake uchumi kwa wananchi unaimarika.
Amewataka wazabuni hao kubadili muda wa ukusanyaji wa taka katika maeneo ya katikati ya Mji badala ya kuzoa taka Mchana, wazoe muda usiku ili waweze kufanya kazi kwa weledi.
Mzabuni MAHOKA TRADING & SERVICES INVESTIMENT atatoa huduma katika kata ya Mjini, Majengo, na Mfaranyaki kwa mawasiliano zaidi 0754-626-840 au 0699-630-033 pia NAMALA II CLEANINGA SERVICES GROUP CO LTD atatoa huduma katika kata za Misufini, Bombambili, na Matarawe kwa mawasiliano zaidi 0715-698-878 au o713- 497-454.
Kwa upnde wa Wazabuni hao wameahdi kufanya kazi kwa umakini bila kukwamisha utekelezaji wa Mkataba husika,
Mikataba hiyo itamudu katika kipindi cha mwaka 2023/2024.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa