Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa walimu katika kusimamia zoezi la utaoji wa chakula kwa wanafunzi shuleni ili kujenga ufanisi wa ufaulu kwa wanafunzi.
Akizungumza na wazazi wa wanafunzi hao katika tafrija fupi ya Mahafali ya kidato cha nne iliyofanyika tarehe 17 Oktoba 2023 shuleni hapo, alisema” Kila mzazi anawajibu wa kuhakikisha mtoto wake anamchangia mchango wa chakula cha shule kwani kutomchangia mchango huo kunadhorotesha maendeleo ya elimu kwa mwanafunzi.” Alisisitiza”
Mhe. Mbano akijibu changamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemo na uchangakavu wa madarasa, uhaba wa vyoo kwa wasichana na wavulana, utoro wa wanafunzi, wazazi kutochangia chakula, uhaba wa viti na meza pamoja na vifaa vya maabara ambapo alisema Halmashauri imeweka bajeti ya shilingi Mil 15 kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya shule.
Akitoa shukrani kwa Jeshi la Wananchi JWTZ kwa kutoa vifaa vya kuzalishia mitihani na kazi nyingine za kitaaluma, pia kwa kukarabati madarasa na kuinua jengo la Utawala hadi kupaua na kuiweka madirisha ambapo aliahidi kununua vifaa na kuikabidhi JWTZ ili wawewze kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala.
Kwa upande wake Mhe. Mathew Ngalimanayo alitoa shgukrani kwa JWTZ kwa ushirikiano wanaoutoa katika kuhakikisha Shule ya Msingi na Sekondari Mashujaa ina kuwa na miundombinu bora na wezeshi katika utoaji wa Elimu.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalin
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa