Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano ameongoza watumishi wa Manispaa ya Songea wakiungana na Madiwani katika kuadhimisha sherehe ya kumuaga na kumkaribisha Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo.
Sherehe hiyo imefanyika tarehe 04 Mei 2024 katika ukumbi wa Chandamali ambayo ilihudhuriwa na Dkt. Sagamiko ( Mkurugenzi muaga) na Adv. Muhoja Mkurugenzi aliyehamia, Viongozi mbalimbali, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watumishi, na waheshimiwa Madiwani iliyofanyika kwa lengo la kumuaga Mkurugenzi wa awali na kumkaribisha Mkurugenzi mpya.
Akizungumza Mhe. Mbano alisema “ alianza kwa kumshukuru mwenyezi mungu kwa maisha aliyoishi Dkt. Sagamiko na hadi kuondoka kwake na pia alimshukuru mungu kwa kutupatia Adv, Muhoja.” Alishukuru”
Akimzungumzia Dkt. Frederick Sagamiko Nanukuu; akisema furaha ambayo unaiona ni matunda uliyoyapandikiza na kuyawekeza kwa watumishi wako hawa katika kipindi chote ulichukuwa ukiishi Songea na hadi leo unaondoka kuelekea Jiji la Tanga tunakuombea safari njema katika utumishi wako pia alimkaribisha Adv. Muhoja.” Mwisho wa kunukuu.
Amewataka watumishi kumpa ushirikiano Adv. Muhoja sambamba na kuchapa kazi kwa bidii ikiwemo na kukamilisha miradi ya maendeleo inayoendelea kujengwa pamoja na kuongeza jitihada za ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Kwa upande wake Adv.Bashir Muhoja alianza kwa kutoa shukrani kwa watumishi wa Manispaa ya Songea kwa kuandaa sherehe kubwa ya kumkarisha katika Halmashauri hiyo. “Alishukuru”
Adv. Muhoja alisema Utumishi ni mabadiliko ambayo hupelekea kuhama kutoka kituo kimoja cha kazi kwenda kituo kingine, ambapo amehaidi kutoa ushirikiano kwa watumishi pamoja kuendeleza shughuli zote alizokuwa akizifanya Mkurugenzi aliyehama na hatimaye Songea kuwa Jiji.
Kwa upande wake Dkt. Frederick Sagamiko alianza kutoa shukurani kwa waheshimiwa Madiwani kwa kumpa ushirikiano wakutosha, Wakuu wa idara na Vitengo, Vyama vya Siasa na Menejimenti yote ya watumishi wa umma kwa kuandaa kwa kuthamini na kutambua uwepo wake katika kipindi cha uongozi wake na hatimaye kuweza kuandaa tafrija ya kumuaga. “ Aliwashukuru’
Dkt. Sagamiko aliongeza kuwa, Katika kipindi chote cha uongozi wake Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini hakijawahi kuingilia au kuonyesha mabavu kwenye maamuzi yanayofanywa na Baraza la Madiwani. Alibainisha.
“Alisema katika furaha inayofurahiwa leo iliyojengwa na jumuiya hii ambayo imechagizwa na watumishi wenzangu ambayo naamini imejengwa katika mambo mawili ambayo ni jumuiya hii kukubali kunichukulia madhaifu yangu mimi kuwa sehemu ya maisha yao, pili walikubali kuyatambua na kuyatangaza mazuri madogo yaliyofanywa na namimi.” Ahsanteni’
Amewataka wakuu wa idara na Vitengo kuendelea kutoa ushirikiano kwa watumishi walio chini yao kwakuwa kila Taasis hakuna mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi peke yake kila mtumishi amewekwa kulingana na muundo wa Serikali, kila mtu aliyeko kwenye muundo amewekwa kwa namna ya utendaji wake huku akiwataka kushirikiana bila kujali nafasi ya mtu. “alisisitiza.”
Mwisho alitoa neno la kuwaaga.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa