Siku ya wazee Duniani ni siku ambayo huadhimishwa ifikapo tarehe 01 Oktoba ya kila mwaka Duniani kote ambapo kwa mwaka 2023 Manispaa ya Songea sherehe hizo zimefanyika tarehe 11 Oktoba 2023 katika viwanja vya Soko kuu Songea Mjini.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile ambayo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali, wananchi pamoja na Wazee kwa lengo la kuhamasisha jamii na kuijengea uelewa na kuwapa hamasa jamii kuhusu kulinda haki, ustawi, na maslahi ya Wazee hapa nchini.
Akizungumza Viwanjani hapo Mhe. Kapenjama Ndile alisema “ Tunatambua kwamba wazee ni rasilimali kubwa ya Taifa hasa katika kipindi cha Changamoto kubwa ya Mmomonyoko wa maadili katika jamii, wakiamini kuwa Wazee wanaweza kuisaidia jamii katika kukabiliana na uvunjifu wa maadili.” Mwisho wa kunukuu.
Aidha, katika kuwatambua Wazee na kupata takwimu sahihi za Wazee kwa Manispaa ya Songea, ina jumla ya Wazee 2144 wanaume, na 1343 wanawake pia katika kuhakikisha wazee wanapata huduma za matibabu, kwa mwaka 2023/2024 jumla ya Wazee 1945 ikikwa Wanaume 837 na wanawake 1,108 wamepatiwa msamaha wa matibabu.
Ameitaka jamii kutekeleza wito kwa kuwajali wazee pamoja na kutambua haki zao za kiuchumi, na kisiasa pamoja na kuwaenzi wazee kwa kuwapatia nafasi ya kutoa maamuzi katika Nyanja za jamii.
KAULI MBIU;
Uthabiti wa Wazee kwenye Dunia yenye Mabadiliko.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa