Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile amewataka Maafisa watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanasimamia kwa uthabiti utekelezaji wa Mkataba wa lishe ili upimaji wa afua za Lishe uweze kufikia leo linakubaliwa.
“Alisema suala la chakula kwa wanafunzi ni jukumu letu viongozi hususani ngazi ya Halmashauri, Kata/Mitaa, shule pamoja na Wazazi wenye watoto shuleni wahakikishe wanafunzi wote wanapata chakula bora kwa lengo la kuleta maendeleo mazuri katika afya ya akili, kimwili, kuimarisha kinga za mwili, na kuzuia magonjwa nyemelezi pia kupelekea kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu katika shule husika.”
Aidha, Wajibu wa viongozi ni pamoja na kuijulisha jamii kuwa, hali nzuri ya lishe inatokana na ulaji wa Mchanganyiko kutoka makundi matano ya chakula na siyo chakula cha aina moja. “ Alibainisha”
Hayo yamejiri wakati wa kikao cha tathimini cha utekelezaji wa Mkataba wa lishe katika kipindi cha Januari hadi Machi 2024 kilichofanyika tarehe 21 Mei 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambacho kilihudhuriwa na Maafisa Watendaji wa Kata pamoja na wakuu wa idara mbalimbali kwa lengo la kufanya mapitio ya utekelezaji wa afua za Lishe Manispaa ya Songea.
Akizungumza Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtela Mwampamba alisema “ Tunapoendelea kuimarisha Klabu za Lishe ni lazima tuhakikishe tunaimarisha klabu hizo kwa kufanya kazi kwa vitendo ikiwemo na uanzishaji wa bustani za lishe kwa shule za Msingi na Sekondari kwa lengo la kupata virutubisho vya lisho bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Adv. Bashir Muhoja amewataka Maafisa watendaji wa Kata, Wakuu wa shule za Msingi na Sekondari wahakikishe wanasimamia uanzishaji wa bustani za mboga mboga na matunda kila shule, kuimarisha klabu za lishe na ushiriki wa wazazi katika kuhakikisha mtoto anapata chakula bora awapo shuleni, Pia ametoa wito kwa wazabuni wote wanaosambaza chakula shueni wahakikishe wanapeleka chakula chenye viini lishe.
Alisema elimu ya uzazi iendelee kutolewa kwa wazazi kabla ya kushika ujauzito wapewe elimu ya afya ya uzazi ili iwasaidie kufanya maamuzi sahihi ya kuzaa kwa umri ulio sahihi na kuzaa mtoto mwenye afya njema na mwenye uzito kamili. “ Adv. Alisisitiza.”
Akiyataja mafanikio ya jumla katika utekelezaji wa Mkataba wa lishe ni pamoja na kuongezeka kwa viwanda vinavyosindika unga wa mahindi na kuongeza viinilishe kutoka 71% hadi 77% kwa sasa, kuendelea kufanya SALIKI ya Kta na Mitaa kwa kuzingatia miongozo, kuongezeka kwa shule za Msingi na Sekondari ambazo wanafunzi wake hutumia unga ambao umeongezwa virutubisho ( Fortified maize flower) kutoka 5.8% hadi 10.9% kwa sasa, kuongezeka kwa wanafunzi wanaopata chakula angalau fvfggggmlo mmoja wanapokuwa shuleni kutoka 53% hadi 62.6% hadi sasa. Alibainisha.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa