Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma, Mheshimiwa Kelvin Mapunda, amewataka Wataalamu wa Afya wa Hospitali ya Madaba Kuendelea Kutunza Miundombinu na Kutoa Huduma Bora kwa Wananchi
Kauli hiyo imetolewa na kiongozi huyo wakati wa ziara ya ALAT Mkoa wa Ruvuma, ambayo ilifanyika tarehe 4 Desemba 2024 ambapo ziara hiyo ilijumuisha ufuatiliaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Madaba, ambapo viongozi hao walipata fursa ya kutathmini maendeleo ya miradi ya afya na miundombinu inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Mapunda alieleza umuhimu wa wataalamu wa afya katika kuhakikisha huduma za afya zinaendelea kwa ufanisi, huku wakizingatia na kutunza miundombinu ya hospitali ili kuhakikisha huduma zinapatikana kwa ufanisi zaidi.
Aidha, alilipongeza taifa kwa jitihada zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha miundombinu ya afya, elimu, maji, barabara, na huduma nyingine muhimu.
Akijibu baadhi ya changamoto zilizoainishwa katika taarifa iliyosomwa naMganga Mfawidhi wa Hospitali ya Madaba, Dkt. Chacha Wambura, Mheshimiwa Mapundaalisema kwamba Serikali inaendelea na jitihada za kuajiri watumishi wa sektambalimbali, hususan wataalamu wa afya, ili kukabiliana na changamoto yaupungufu wa wafanyakazi katika hospitali za umma ambapo alisisitiza kuwawananchi wanapaswa kuwa na subira wakati Serikali ikishughulikia changamotohizo kwa kadri inavyowezekana.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Madaba, Dkt. Chacha Wambura, alieleza kuwa hospitali hiyo ilianza kutoa huduma kwa wananchi mnamo tarehe 19 Septemba 2023, ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje, kliniki ya baba, mama na mtoto, huduma za maabara, huduma za dharura na ajali, huduma za wagonjwa wa ndani, ustawi wa jamii na lishe, huduma za uzazi (kawaida na upasuaji), huduma za upasuaji mdogo, huduma ya kinywa na meno, pamoja na huduma ya kuhifadhi maiti.
Hata hivyo, alibainisha kuwa hospitali hiyo inakutana na changamoto ya upungufu wa watumishi, ambapo mahitaji ya wafanyakazi ni 200, lakini hadi sasa watumishi waliopo ni watumishi 27 pekee.
Ziara hiyo ya ALAT Mkoa wa Ruvuma ilihudhuriwa na wajumbe wa jumuiya kutokahalmashauri zote za mkoa wa Ruvuma, wakiwemo wenyeviti wa halmashauri, naibumeya, na wakurugenzi kutoka halmashauri nane za mkoa huo.
Ziara hiyo ya ALAT Mkoa wa Ruvuma ilihudhuriwa na wajumbe wa jumuiya kutokahalmashauri zote za mkoa wa Ruvuma, wakiwemo wenyeviti wa halmashauri, naibumeya, na wakurugenzi kutoka halmashauri nane za mkoa huo.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa