NA;
AMINA PILLY – Mwandishi wa ALAT Mkoa wa Ruvuma.
Jumuiya za Tawala za Serikali za Mitaa (ALAT) Mkoa wa Ruvuma wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya Namtumbo ambapo walitembelea mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na matundu 6 ya vyoo uliopo katika kijiji cha Mkongo pamoja na Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa Dkt. Samia Suluhu Hassan .
Akizungumza Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma Kelvin Mapunda alisema lengo la ziara ni kutembelea miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Namtumbo, kujifunza na kupeana uzoefu wa uendeshaji wa shughuli za maendeleo.
Aidha, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya uendeshaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo miundombinu ya elimu, Afya na nyinginezo. “Alipongeza”
Mhe. Mapunda amewapongeza wananchi wa kata ya Mkongo kwa kujenga madarasa mawili 2 katika shule (shikizi) ya Mkongo ambayo imejengwa kwa gharama ya Mil. 26 kati ya hizo mil 20 ni nguvu za wananchi, na mil 6 ni fedha za mfuko wa jimbo.
Ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kuhakikiksha wanakamilisha ujenzi wa madarasa hayo ili yaweze kupunguza mrundikano wa wanafunzi darasani, pia itasaidia kupunguza umbali mrefu, pamoja na kuchochea ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi kutokana kutokuwepo kwa utoro wa shule. “Alibainisha.”
Akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyopo Wilayani humo ambapo amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii, kuwa na nidhamu, utii na kumcha Mungu katika kipindi chote cha masomo yao.
ziara hiyo imefanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 15 hadi 16 Aprili 2024 ambayo ilihudhuriwa na Wenyeviti wa Halmashauri 7, Mstahiki Meya, Wakurugenzi wa Halmashauri 8, Waheshimiwa Madiwani 2 wawili kutoka kila Halmashauri pamoja na waandishi wa vikao wa Halmashauri.
Akisoma taarifa Mwl Dafrosa Chilumba Mkuu wa shule ya wasichana ya Mkoa Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema awamu ya kwanza Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa Dkt. Samia Suluhu Hassan ilipokea fedha kiasi cha Tsh 3,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 12, mabweni 5, maabara 4, jengo la utawala 1, nyumba ya walimu 2 moja, nyumba ya matroni 1, vyoo matundu 16, pamoja na Bwalo 1 na ujenzi umekamilika.
Awamu ya pili Shule ilipokea Bil. 1,100,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 10, jengo la TEHAMA 1, maktaba 1, nyumba 2 za walimu 2, nyumba ya vyumba 3 moja, pamoja na mabweni 4 ambapo baadhi ya miradi imekamilika na miradi mingine ipo hatua ya ukamilishaji. “Alibainisha.”
Kwa upande wa wanafunzi wa shule ya wasichana ya Mkoa Dkt. Samia Suluhu Hassan wametoa shukrani kwa Serikali kwa kujenga shule ya Wasichana ya Mkoa ambayo itawezesha kusoma katika mazingira mazuri na wameaahidi kufanya vizuri katika masomo yao.
"MWISHO."
.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa